Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Baadhi ya watu wa chama cha kijani wanatumia nguvu kubwa na muda wao mwingi kufanya kila waliwezalo kuhakikisha Mbowe harudi madarakani iwapo ataamua kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Binafsi watu hawa nawasikitikia sana kwani huenda hawajui walitendalo mithili ya wale Wyahudi waliomsulubisha Yesu msalabani ambao nao walikuwa hawajui walitendalo.
Na vita hii dhidi ya Mbowe bila shaka ina baraka za watu wakubwa tu walioko katika chama cha hawa wenzetu na pengine wana lengo la kutaka kutumia uchaguzi huo kuweka pandikizi lao katika nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa masilahi yao ya kisiasa kama wanavyotuhuimiwa kuweka mapandikizi katika baadhi ya taasisi au vyama na kuzifanya taasisi au vyama hivyo kuwa ni taasisi butu/mfu.
Mimi nawashauri watu hawa wajue tu kuwa ikitokea Mbowe harudi madarakani kwa yeye mwenyewe kutogombea au vinginevyo, huku jitihada za kuweka mwenyekiti pandikizi zikifeli na badala yake CHADEMA wakafanikiwa kupata mwenyekiti mpya atakaekuja na misimamo na mitazamo tofauti katika kuiongoza CHADEMA ikiwamo kukataa kuvumilia uonevu huu unaoendelea dhidi ya wana-CHADEMA na upinzani kwa ujumla,basi watu wa chama cha kijani wajue tu wanaweza kuja kukumbuka sana Mbowe na wanaweza kuja kujuta na kusema bora Mbowe angebaki tu kuiongoza CHADEMA.
Busara na uvumilivu wa Mbowe, hamtaweza kuviona sasa mpaka pale mtu mwingine atakapochukua nafasi yake ingawa teyari Spika hivi karibuni alikiri kuwa Mbowe ni mtaratibu akimlinganisha na Lissu aliemuoma ni mtu mkorofi/mwenye kiburi.
Turejee maneno ya wahenga: "mtoto akililia wembe,mpe".