Laptop Yako Inapumua Kama viumbe vingine.
Laptop yako inahitaji kupumua kama binadamu na viumbe wengine. Inahitaji kuingiza hewa na kutoa hewa ili iweze kufanya kazi vizuri na kudumu kwa muda mrefu.
Kwa matumizi ya kawaida laptop ilitengenezwa kuweza kupumua juu ya meza lakini unapoiweka laptop yako kitandani juu ya shuka, mto au blanketi, inapata shida kubwa ya kupumua. Hii inatokana na airflow (mtiririko wa hewa) ya laptop, ambayo ni muhimu kwa ufanisi na kudumu kwa kifaa.
Jinsi laptop inavyoumua
Laptop ina mashimo kwa chini ambayo huingiza hewa (air intake) na mashimo ya kutoa hewa (air exhaust) pembeni au nyuma karibia na feni.
Jukumu la Feni
Feni ni kama mapafu ya laptop. Inavuta hewa baridi kutoka chini na kuisambaza kwenye vifaa ambavyo huzalisha joto kama Processor, hard disk, rama na vinginevyo. Hii husaidia kupunguza joto (cooling) na kuhakikisha kuwa laptop inafanya kazi kwa ufanisi na kulinda vifaa visiharibiwe na joto.
Baada ya kuzungusha hewa baridi, feni inasukuma hewa yamoto nje kupitia mashimo ya pembeni au nyuma (exhaust).
Ikiwa unaiweka laptop yako kitandani, matundu ya chini yanazibwa, na hewa haiwezi kuingia vizuri. Hii inasababisha laptop kupata joto kupita kiasi, na feni kushindwa kufanya kazi vizuri. Matokeo yake ni:
- Utendaji duni: Laptop itahitaji nguvu zaidi kudhibiti joto, hivyo kufanya kazi kwa upolepole.
- Joto kupita kiasi: Joto linalozalishwa na vifaa vya ndani kama halidhibitiwi vizuri laptophuwa inapata joto sana
- kuharibu laptop yako: kama joto halidhibitiwi vizuri linaweza kuchangia kuharibika kwa vitu vingi uanze kuhangaika kwa mafundi au kugharamika kununua vifaa vipya.
Suluhisho: Nunua stendi
Ikiwa unataka laptop yako ifanye kazi vizuri, idumu na kupunguza joto ni muhimu kuzingatia airflow yake. nunua stendi inainua laptop yako kidogo juu ya shuka au blanketi, na hivyo inaruhusu airflow.
Bei ya stendi ya kawaida ni elf 20.