Mnaotumia simu ya laini moja na kutembea na ya ziada kwa laini ya pili huwa hamuoni unafuu kutumia simu zenye laini 2?

Mnaotumia simu ya laini moja na kutembea na ya ziada kwa laini ya pili huwa hamuoni unafuu kutumia simu zenye laini 2?

Duh
Kama jambazi mzee
Inalazimika kwa mfano sisi maafisa ubashiri huwa hatupendi zile message za mikeka au matangazo ziingie kwenye namba ya kawaida inayojulikana na wife, anawaka.
 
Hatuoni mzigo

Binafsi hiko kiswaswadu nakigusa mpaka nisikie kinaita.. kama hakijaita naweza shtuka kimezima chaji
 
Mimi nina simu 2 laini 5.
  • Simu ya kwanza laini 3,
  • simu ya pili laini 2.

Matumizi yake sasa
° Laini 2 zinajulikana na watu wote. Mojawapo ya hizi nimesajililia sehemu kama email, bank, nida, kwenye CV nk. Hizi muda mwingi hewani.
° Laini ya 3 inajulikana na watu wote isipokuwa kazini. Nikiamua, nawazimia kazini laini 2 za hapo juu halafu naendelea na mishemishe mtaani huku mawasiliano yakitumika kwa laini hii ya 3. Nikiibuka nasema nilikuwa shamba huko.
° Laini ya 4 nikitongoza demu au mtu ambaye sitaki mawasiliano naye baada ya kazi fulani mfano polisi nk. ndio nampa hiyo namba. Hiyo kuizima muda wowote sionagi kazi hata siku 5.
Hii pia ndio naitumia kama afisa ubashiri.
° Laini ya 5 ni Lipa namba. Hii simpigii mtu yeyote, hata nikipigiwa najua ni wrong number, nitajibu tu umewrong.

Nalinda sana mawasiliano.
Siwezi kumpigia mtu kwa namba ambayo haimhusu. Hata kama nimeishiwa salio na nina salio kwenye namba isiyokuhusu, nitajitahidi niunge kifurushi kwa namba husika.
Ww ni tapeli
 
Ww ni tapeli
Hata sio utapeli. Hapo laini za matumizi ni 4, ya 5 ni miamala tu.
Je kuwa na laini 4 ni utapeli?
Laini 2 mawasiliano ya watu wote
Laini 1 watu wote isipokuwa kazini.
Laini 1 ni kama namba ya dharura, wanapewa mademu, polisi, kubeti nk.
Ukifanya hivi hakuna siku wife atakushitukia kama unachepuka. Maana mchepuko unaupa namba maalum, ukifika home unazuia kwa ussd msg zisiingie, kisha unachomeka simu charge unawambia wife zikijaa achomoe kisha wewe unaenda kucheza draft huko.
Hata achunguze vp hakupati.
 
Back
Top Bottom