Mimi nina simu 2 laini 5.
- Simu ya kwanza laini 3,
- simu ya pili laini 2.
Matumizi yake sasa
° Laini 2 zinajulikana na watu wote. Mojawapo ya hizi nimesajililia sehemu kama email, bank, nida, kwenye CV nk. Hizi muda mwingi hewani.
° Laini ya 3 inajulikana na watu wote isipokuwa kazini. Nikiamua, nawazimia kazini laini 2 za hapo juu halafu naendelea na mishemishe mtaani huku mawasiliano yakitumika kwa laini hii ya 3. Nikiibuka nasema nilikuwa shamba huko.
° Laini ya 4 nikitongoza demu au mtu ambaye sitaki mawasiliano naye baada ya kazi fulani mfano polisi nk. ndio nampa hiyo namba. Hiyo kuizima muda wowote sionagi kazi hata siku 5.
Hii pia ndio naitumia kama afisa ubashiri.
° Laini ya 5 ni Lipa namba. Hii simpigii mtu yeyote, hata nikipigiwa najua ni wrong number, nitajibu tu umewrong.
Nalinda sana mawasiliano.
Siwezi kumpigia mtu kwa namba ambayo haimhusu. Hata kama nimeishiwa salio na nina salio kwenye namba isiyokuhusu, nitajitahidi niunge kifurushi kwa namba husika.