Mnapata wapi Marafiki Physically?

Mnapata wapi Marafiki Physically?

Kunywa pombe, shabikia mpira, nenda kanisani

Life is good with friends. Ila kwenye pombe ckushauri sana
 
Ndio ila SIO kila mtu anae enda kanisan anaweza kuwa rafiki mwema na matapel wamo[emoji28]
Kuna kipindi nilikuwa kama huyu mleta mada nilikua mahudhuria kanisani kila siku lakini ndio kama nilizidi kuwa mpweke.
 
Pamoja mkuu. Ngoja nitaanza basi sema hobbies zangu ni changamoto kidogo.

Naangalia Formula 1 na Motor GP na naangalia movies sana.

So outings zangu sana sana ni cinema tu. Nimejaribu Bar dah nimeshindwa.

Nitajaribu Mpira niwe mshabiki wa timu local na nje moja.
uwez kushindwa ,jikazee
 
Mtoa mada tunachohitaji ni kuishi na watu vizuri.

Kuwa na rafiki sio lazima,muhimu ishi na watu vizuri kiasi kwamba hata ukianguka chumbani uweze kupiga simu upate watu wa kukupeleka hospitali
 
Hivi nyie wenye marafiki ambao mnatembeleana na kukutana physically weekend mnawapata wapi?

Mbona mi niko mwenyewe sana Yaani weekend nazichukia bora weekdays nikiwa kazini muda unaenda ila weekend niko mwenyewe kama zombie.

Nijichanganye wapi na mimi nijuane ata na washkaji wawili watatu. Kwenye simu ninao wana wengi sana tunaweza chat ata masaa 100, ila physically sio kabisa.

Sinywi pombe, sio mshabiki wa mpira, siendi kanisani.. Nipo nipo tu
Kawaida tu mkuu,
Mimi kama wewe tu,ila najisikia normal tu.. Halafu nakuwa comfortable nikiwa pekeyangu..
 
Back
Top Bottom