Mnapoongozwa na Dola Ovu

Mnapoongozwa na Dola Ovu

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Mhalifu au mwovu huweza kuwa mtu binafsi, serikali/dola, taasisi, kikundi rasmi au kisicho rasmi. Uovu mbaya kabisa ni ule wa dola maana huo unafanywa dhidi ya wananchi ambao kihalisia walistahili kuheshimiwa na kutendewa haki.

Wanaosababisha dola iwe ovu ni watawala waovu. Na bahati mbaya sana, ikitokea mkipata watawala waovu, watatumia nguvu za kidola kukamilisha uovu wao. Huo ni uovu mbaya sana kwa sababu ni ngumu sana kupambana nao maana waovu wanakuwa na vyombo vya dola, pesa ya umma, na hulindwa na sheria walizotengeneza ili kulinda uovu wao.

Dola inapokuwa ovu, huvilazimisha vyombo vingine vyote vitende uovu. Dola italilazimisha bunge liwe la kiovu na mahakama nayo iwe mahakama ovu. Vyombo vya dola, kama polisi, idara za usalama na intelijensia, vyote hutumikia uovu. Ikishafikia hapo, mwananchi anakuwa hana kimbilio. Atakamatwa na polisi, atapigwa, atateswa, ataporwa, anaweza hata kuawa. Akienda mahakamani, anakutana na mahakama ovu, nayo itamfunga maana ni serikali ile ile ovu huwa imeweka mahakimu na majaji wake waovu. Na bungeni kutatungwa sheria za kulinda uovu.

Dola ovu hupenda sana kuitumia mahakama (mahakama ovu) ili kuhadaa, ili ule ouvu usionekana kwa udhahiri, ionekane ni maamuzi ya mahakama. Madikteta wote hujificha nyuma ya mahakama na Bunge.

Chini ya mfumo wa dola ovu, waovu, watu wasiotenda haki, hutuzwa, hupongezwa na huzawadiwa. Yaani yule mwovu zaidi kwa nia ya kutekeleza matakwa ya watawala waovu, ndiye mwenye nafasi kubwa kupandishwa cheo na kupewa maslahi mazuri zaidi kuliko watenda haki.

Kukiwa na Serikali ovu, kadiri inavyokaa madarakani kwa muda mrefu, ndivyo inavyozidi kuweka mizizi ya uovu kila mahali. Kuiondoa dola ovu, na kazi ngumu kwa sababu mizizi ya uovu huwa imegusa karibia taasisi zote. Hata kwenye taasisi za huduma kama elimu na tiba, haziponi. Mashuleni na vyuoni, wanafunzi watapofushwa ili wakati wote waiabudu dola ovu. Hospitalini, watu wanaweza kufanyiwa ovu, kama mazingira mengine hayakuruhusu anayetakiwa kutendewa uovu kuweza kutendewa uovu.

Dola ovu hudumaza akili za watu. Huwalisha ujinga ili wawe waimba mapambia ya kutukuza dola ovu.

Sifa kubwa mojawapo ya dola ovu ni kupenda kusifiwa, kutafuta sifa za uongo, na kutopenda watu wenye akili na fikra huru.

Jambo la matumaini ni kwamba, mwanadamu kwa asili yake, huchukia na kupingana na uovu. Hivyo dola ovu, japo inaweza kudumu kwa miongo, lazima huja kuondolewa, tena kwa aibu kubwa. Kwa asili mwanadamu ana roho ya itakatifu ila shetani huweza kuchukua na akawa wakala wake, na hapo sasa hamu ya uovu huimarika ndani yake.
 
Kama Magu alikuwa kiongozi muovu sana kiasi kwamba kansa yake ikatapakaa kila mahali kulinda uovu wake. Kwa mara ya kwanza Tanzania tukaanza kuona viongozi kama jaji mkuu na spika nao wanawekewa kinga ya kutoshtakiwa, ili wafanye uovu wao bila wasiwasi. Huko aliko huyo jamaa achomwe Moto mkali zaidi.
 
Hivi kwanini spika alipewa kinga ya kutoshtakiwa?

CCM ni chama kilichofitinika.

Hakifai hata kwa sekunde moja kuwaongoza Watanzania.
 
Hivi kwanini spika alipewa kinga ya kutoshtakiwa?

CCM ni chama kilichofitinika.

Hakifai hata kwa sekunde moja kuwaongoza Watanzania.
Kwa vyovyote, wakati marehemu alipotaka hii mihimili ifanye yaliyo maovu, spika na jaji mkuu walipatwa na hofu. Naye ili kuwahakikishia wasiwe na mashaka yoyote, akaamua kuwalinda kwa sheria zile za kulinda uovu, ili wasishtakiwe hata siku moja wakati walipotumika kulinda uovu wa dola.
 
Back
Top Bottom