Mnapopewa ofa muwe mnaanza kujitathimini

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Yaani mtu umemtoa Lunch au Dinner muwe mnaangalia kwanza mwenyewe kaagiza nini.

Tena jinsia ya KE ndio kabisa huko siwezi kuwazungumiza tujumuishe wote.

Yaani nimetoa jamaa tendwe tukapate supu anaona mimi naagiza makongoro ya ng'ombe yeye anaagiza mchemsho wa kuku tena kidali. Kwa nini usisubiri kusikia muhusika kwanza.

Kuna wengine umeagiza chakula cha kawaida yeye anaagiza kushinda wewe.

Tuheshimiane tutakwepana: Jana nampa mtu ofa chukua bia anaona nakunywa balimi yeye anataka Windock tena anabugia kwa sifa.
 
Tunaomba radhi kwa wale wote watakaokwazika mwandishi ni mmoja wa wagonjwa wetu katika hospital ya crazy for life.

Ndugu chizcom , alifanikiwa kutoroka jana na kuiba simu za ofisi na Sasa anaropoka hovyo tu.

Tunashukuru kwa ushirikiano wenu na tunaahidi tutalishughulikia swala hili hivyo mvumilieni.

Naambatanisha ushahidi wa vyeti alivyovipata kutoka hospital
 
Kutoa ofa sio lazima bro ukiona mfuko wako huuelewei kausha tu usimkaribishe mtu
Hujaona hoja hata moja mkuu?
Jamaa kaongea vizuri mkuu.
Ukialikwa chukua tahadhari usijiachie sana.

Yesu alisema ukilikwa karamuni kaa viti vya nyuma...subiri uletwe viti vya mbele.

Lengo ni nini?.
Ikiwa nimekualika halafu ukaagiza chakula cha bei ndogo labda kwa uoga...mimi niliyekualika nitakwambia chukua hata kuku mzima na wine.

Na kama siko poa hicho hicho cha bei ya kawaida nitakuacha uendelee nacho.

Mimi niliwahi kumtoa mtu out aliagiza vinywaji na chakula jumla 300k.
Je kama ningekuwa mchovu unafikiri ingekuwaje?
 
Ujinga wa bier ni huu. Unaondoka zako peke yako unaagiza bia zako mbili. Kama uliweka dhamira unywe mbili, sasa ukiisaliti dhamira yako ukanywa tatu basi dhamira nayo ina revenge, payback tyme! Unajikuta unatoa simu mwenyewe mfukoni unatafta wana, ooy wewe fisi maji uko wapi? Umbwa wewe njoo unywe mbili, unatafta mwingine na mwingine na mwisho wa siku unajikuta meza ina watu kama saba imetapika vyupa huku mlipaji ukiwa ni wewe. Pesa yako inakusaliti. Hukomi, siku ingine unarudia upuuzi ule ule, i quit
 
Sasa umempa ofa kisa nini??
 
Ukimualika mtu sehemu ya 5star hakikisha mfuko wako umevimba...
Ukiona uko mbaya mualike kwenye grocery au usialike mtu kabisa.
Mialiko na masharti wapi na wapi? Lakini pia wabongo tunajistukia... Niliwahi waalika watu kwa ajili ya mazungumzo fulan kwenye hotel ya 3* nikawaweka huru kwamba wale chochote maana ile meeting ilikuwa yangu... Huwezi amini waliogopa wakanihurumia kwamba hawawezi kutokana na bei kuwa kubwa.

So mnapoita watu hakikisheni mifuko yenu imevimba la sivyo jibaneni wenyewe
 
Ila bloangu inaonekana una hali ngumu sana,yaani hata tuchakula ka let say tu-elf10 unakuja kuanzisha uzi kabisa humu bloangu kweli?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…