Mnapopigana "vibuti"...

Kate, wewe inaelekea ushawahi pitia drama kibao kwenye mahusiano yako...


Kwa sana tu NN,siku hizi mtu akianza tu kubadilika najua anakoelekea,taratibu najiweka pembeni huku nikimtizama,

i
 
Kwa sana tu NN,siku hizi mtu akianza tu kubadilika najua anakoelekea,taratibu najiweka pembeni huku nikimtizama,

i

Hahahaaa duuuuh wewe kiboko. Mzima lakini? Siku hizi umekuwa adimu kama almasi!
 
aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa umenikumbusha kitu kuna rafiki yangu alisomeshwa na mpenzi wake baadae wakagombana na kuachana jamaa akamwambia naomba unirejeshee gharama zote nilizokuwa nakupatia ikiwa pamoja na cm aliyomnunulia,duh myfrnd akamwambia hayo yalikuwa ni mapenzi siwezi kukurudishia.
kwenye mada........huo ni ushamba wa hali ya juu sana kama amekudhurumu Mungu atamuhukumu kwa haki yake.
 
Kama kulikuwa na mapenzi ya kweli kati yenu na sio usanii basi sioni sababu ya kunyang'anyana zawadi.

 
Last edited by a moderator:
Dada /Mama.. u make sense. Unajua chimbuko la matatizo yote uyaonayo duniani hapa ni "UBINAFSI". watu hapa jamvini wanatoa ushauri wakiwa na ubinafsi huo huo. Linapokuja jambo kama hili akina dada wanatoa maoni yanayowafurahisha mioyo yao,hali kadhalika akina kaka/baba. Ningependa kusikia mwanadada aliyemnunulia gari boyfrnd wake,then huyo kijana alete nyodo na kujiona matawi,na kwa gari hilo hilo alitumie atongozee wanawake wengine ,then utajisikiaje,? Atamwachanalo??. kwa hivi ushaurimwingine utolewao hapa ndani ni wa kujifurahisha na ushabiki zaidi. Vitu ambavyo huwezi kudai ni hivi vya kawaida. Au tuseme kwa ujumla INATEGEMEA NA HALI HALISI YA KUACHANA NA ZAWADI/VITU MLIVYOPEANA.Period.
 
true! mi nilishushwa kwenye kivits mchana kweupeee posta!!
ningekuwa mimi sishuki yani pangechimbika na ningefunga mataa mwanaume akikuletea za kuleta usicheze mbali onyesha gender equality hapo mm angekimbia mwenyewe bila kukimbizwa
 
Ni ushamba wa hali ya juu kama sio ulimbukeni kudaiana vitu mlivyopeana wakati mkiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi! Tena ni umasikini wa roho!

Hata ile gari yangu RAV 4 niliyomnunulia nisiidai????? Thubutuuuuuuuuuuuu
 
ningekuwa mimi sishuki yani pangechimbika na ningefunga mataa mwanaume akikuletea za kuleta usicheze mbali onyesha gender equality hapo mm angekimbia mwenyewe bila kukimbizwa

Weeeeeee ungeona dunia chungu na ungetamani ardhi ipasuke. Katafute kwingine au kanunue yako, tena ningewaambia polisi hiyo gari niliibiwa jana usiku!!
 
Duh mi ni lidaiwa mpaka elfu kumi niliyowahi kupewa, kisa nakipiga kalenda kijitu kila siku, sitoi jibu nadanganya tu. Ha haaaa. Kuna watu wanaroho za kimaskini sana, na watu wa hivyo waangalie wote hua wanafanana, hua hawana maendeleo hata angesomaje hata elimu yake haiwezi msaidia.
 
katika uchumba/mahusiano ya kimapenzi inatokea kufarakana hata kuachana...je vile vitu mlivyokua mkipeana enzi hizo (zawadi,..picha) yapasa mrudishiane?..

kila mmoja abaki na souvenir yake..................................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…