Mnaposema Dar es Salaam itapata maji 100% ni ipi hiyo? Ile ya Mabwanyenye wa CCM na washirika wao? Vipi madongo poromoka kama Buza na Mbagala?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Nina hakika mtandao maji ya Dawasa haujtandaa Dar yote.

Ni baadhi ya maeneo tu ndio kuna mtanado huo

Sasa hao wanaokaaa madongo poromoka mnawafikiria vipi na wao?

Mtakuwa mnajaza waterbowser na kuwapelekea?

Ndiyo kusema mnaposema Dar mna maanisha mnapooshi nyie mabwanyenye?
 
Nani kakwambia buza kunashida ya maji? Kuna time msipende Sana kujidai mnaijua buza.
 
JE NI UWEZO MDOGO WA VYANZO VYA MAJI DAR ES SALAAM?

DAWASA watakiwa kufanya kazi usiku na mchana, RC Makalla​

thumb_842_800x420_0_0_auto.jpg
Posted On: October 28th, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla ameuagiza uongozi wa DAWASA kusimamia Mkandarasi anayesimika mabomba ya kusambaza maji kufanya kazi usiku na mchana ili kuendana na matumaini waliyoyatoa kwa wananchi ya kufikishia maji maeneo ya Wilaya ya Kigamboni na Ilala kuanzia Jumatatu ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wake.

Mhe Makalla ameyazungumza hayo leo alipokuwa kwenye ziara yake ya kutembelea visima vya maji vya Kigamboni na kuzindua zoezi la kuwasha maji ya kisima kinachoitwa K11 kinachopeleka maji hayo kwenye Tanki Kuu lenye uwezo wa kuchukua lita milioni 15 za maji lililojengwa Kisarawe II Kigamboni.

Pia aliwaeleza wananchi kuwa Serikali inachukua hatua zikiwemo za dharula na za muda mrefu kukabiliana na upungufu wa maji.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Rais alitoa maelekezo wakati anashughulikia changamoto ya maji, kuwa mradi wa Kigamboni ukamilike kwa haraka kwani alishaidhinisha kiasi cha Bilioni 23 ili kukamilisha mradi kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa maji unaojitokeza kwasasa baadhi ya maeneo.

Aidha ameupongeza uongozi wa DAWASA kuanzia Mkurugenzi, Mwenyekiti wa bodi na watendaji kwa kazi nzuri waliyoifanya, amethibitisha kuwa wanaweza kusimamia na matokeo yake yameonekana.

Ameongeza kuwa Rais anaendelea kuchukua hatua,mchakato wa kupata mkandarasi wa kujenga bwawa la kidunda ambalo kwa kiasi kikubwa litamaliza changamoto ya maji amepatikana na wakati wowote ataanza kazi.

Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa anaishukuru sana Serikali kwa kusaidia na kuiwezesha DAWASA kuweza kukabiliana na changamoto hizo ambazo zimekuwepo na wao kama viongozi wanaendelea kuzitatua hatua kwa hatua.

Mkurugenzi wa DAWASA Eng.Cyprian Luhemeja amesema kuwa kuna visima 7 ambavyo vimekamilika vyenye uwezo wa kutoa lita milioni 70, Mahitaji ya Kigamboni na Ilala ni chini ya milioni 70 hivyo wanaamini baada ya mradi kukamilika changaomoto ya maji kwenye maeneo haya ya Ilala, Kigamboni, Temeke na Kurasini itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa.

IMG_2897.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakifurahi kwa pamoja mara baada ya kuwasha maji kwenye kisisma cha K11

IMG-20221028-WA0010.jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza baada ya kutembelea mradi wa tanki kuu.

IMG-20221028-WA0016.jpg

Tanki kubwa la maji linalokusanya maji kutoka kwenye visima 12 vilivyojengwa Kigamboni.
IMG-20221028-WA0013.jpg

Mkurugenzi wa DAWASA Eng.Cyprian Luhemeja akielezea njia zitakazopita mabomba ya maji yanayojengwa ili kuzifikia Wilaya nyingine za Ilala na Temeke.

IMG-20221028-WA0015.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla akiwa ameambatana na viongozi wengine wakielekea kutazama namna maji yanavyoingia mara baada ya kuwasha kutoka kwenye kisima cha K11.

IMG-20221028-WA0011.jpg

.Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla akiwa ameambatana na viongozi wengine wakishuka kutoka kwenye tanki kuu mara baada ya kutazama namna maji yanavyoingia baada ya kuwasha kutoka kwenye kisima cha K11
Source : DAWASA watakiwa kufanya kazi usiku na mchana, RC Makalla
 
HANSARD Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. AHADI YA VISIMA 2017 / 2018

MHE. LUCY S.MAGERELI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru na nimeshukuru kupata majibu ya Serikali, lakini...

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijauliza maswali yangu mawili ya nyongeza naomba nitoe maelezo mafupi ya utangulizi kwamba ni fedheha na ni mambo ya aibu kabisa kwa Jiji kongwe kama Dar es Salam kwa Mji Mkuu wa biashara wa muda mrefu tangu uhuru wa nchi hii kupatikana kuendelea kuteseka na adha ya maji mpaka leo hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu ya Serikali anazungumzia habari ya visima 20 ambavyo vinachimbwa Mpera na Kimbiji.

Kwa bahati mbaya ni kwamba visima hivyo mpaka sasa havijakamilika kwenye zoezi la kuchimbwa.

Je, fedha wanazosema wanatafuta, zinatafutwa kutoka wapi na zitapatikana lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwenye majibu ya Waziri anasema katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imepanga kukamilisha miradi ya viporo kama kipaumbele.

Tunavyozungumza bajeti 2017/2018 inakwisha siku chache sana zijazo na bado….
Mheshimiwa Mwenyekiti, swala hili linaitwa kipaumbele. Je, Mheshimiwa Waziri anajibu tofauti kwenye swali (b)?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwenyezi Mungu anasema unapaswa kushukuru kwa kila jambo na usipowashukuru binadamu hata Mwenyezi Mungu unaweza hutamshukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kabisa Jiji la Dar es Salam lilikuwa na changamoto kubwa sana ya maji, lakini mpaka sasa asilimia 78 ya wananchi wanapata maji safi, salama na yenye kuwatosheleza.

Watu wa Mamlaka ya DAWASCO wana mpango mkubwa mkubwa wa kuongeza mtambo ile wa Ruvu juu na Ruvu chini katika kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam wanaendelea kupata maji, safi salama na yenye kuwatosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa katika maeneo ya viunga vya Dar es Salam kwenye changamoto ya maji Serikali imeshachimba visima 20 na sasa tumejipanga katika kuhakikisha tunasambaza maji ili wananchi wa Ukonga na maeneo mengine waweze kupata maji safi, salama na yenye kutosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu miradi ya viporo, kazi inaendelea kufanyika, nimuombe Mheshimiwa Mbunge aendelee kutuamini na sisi katika yale maeneo ambapo tunahitajika kukamilisha viporo vile tutaendelea kuvikamilisha kwa wakati, ahsante sana.
Source : Bunge Polis
 
Utasikia wana ccm kwa uwezo mama maji yana pitakana na yakikosekana tuombe mungu
 
JE NI UWEZO MDOGO WA VYANZO VYA MAJI DAR ES SALAAM?

DAWASA watakiwa kufanya kazi usiku na mchana, RC Makalla​

thumb_842_800x420_0_0_auto.jpg
Posted On: October 28th, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla ameuagiza uongozi wa DAWASA kusimamia Mkandarasi anayesimika mabomba ya kusambaza maji kufanya kazi usiku na mchana ili kuendana na matumaini waliyoyatoa kwa wananchi ya kufikishia maji maeneo ya Wilaya ya Kigamboni na Ilala kuanzia Jumatatu ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wake.

Mhe Makalla ameyazungumza hayo leo alipokuwa kwenye ziara yake ya kutembelea visima vya maji vya Kigamboni na kuzindua zoezi la kuwasha maji ya kisima kinachoitwa K11 kinachopeleka maji hayo kwenye Tanki Kuu lenye uwezo wa kuchukua lita milioni 15 za maji lililojengwa Kisarawe II Kigamboni.

Pia aliwaeleza wananchi kuwa Serikali inachukua hatua zikiwemo za dharula na za muda mrefu kukabiliana na upungufu wa maji.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Rais alitoa maelekezo wakati anashughulikia changamoto ya maji, kuwa mradi wa Kigamboni ukamilike kwa haraka kwani alishaidhinisha kiasi cha Bilioni 23 ili kukamilisha mradi kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa maji unaojitokeza kwasasa baadhi ya maeneo.

Aidha ameupongeza uongozi wa DAWASA kuanzia Mkurugenzi, Mwenyekiti wa bodi na watendaji kwa kazi nzuri waliyoifanya, amethibitisha kuwa wanaweza kusimamia na matokeo yake yameonekana.

Ameongeza kuwa Rais anaendelea kuchukua hatua,mchakato wa kupata mkandarasi wa kujenga bwawa la kidunda ambalo kwa kiasi kikubwa litamaliza changamoto ya maji amepatikana na wakati wowote ataanza kazi.

Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa anaishukuru sana Serikali kwa kusaidia na kuiwezesha DAWASA kuweza kukabiliana na changamoto hizo ambazo zimekuwepo na wao kama viongozi wanaendelea kuzitatua hatua kwa hatua.

Mkurugenzi wa DAWASA Eng.Cyprian Luhemeja amesema kuwa kuna visima 7 ambavyo vimekamilika vyenye uwezo wa kutoa lita milioni 70, Mahitaji ya Kigamboni na Ilala ni chini ya milioni 70 hivyo wanaamini baada ya mradi kukamilika changaomoto ya maji kwenye maeneo haya ya Ilala, Kigamboni, Temeke na Kurasini itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa.

IMG_2897.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakifurahi kwa pamoja mara baada ya kuwasha maji kwenye kisisma cha K11

IMG-20221028-WA0010.jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza baada ya kutembelea mradi wa tanki kuu.

IMG-20221028-WA0016.jpg

Tanki kubwa la maji linalokusanya maji kutoka kwenye visima 12 vilivyojengwa Kigamboni.
IMG-20221028-WA0013.jpg

Mkurugenzi wa DAWASA Eng.Cyprian Luhemeja akielezea njia zitakazopita mabomba ya maji yanayojengwa ili kuzifikia Wilaya nyingine za Ilala na Temeke.

IMG-20221028-WA0015.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla akiwa ameambatana na viongozi wengine wakielekea kutazama namna maji yanavyoingia mara baada ya kuwasha kutoka kwenye kisima cha K11.

IMG-20221028-WA0011.jpg

.Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla akiwa ameambatana na viongozi wengine wakishuka kutoka kwenye tanki kuu mara baada ya kutazama namna maji yanavyoingia baada ya kuwasha kutoka kwenye kisima cha K11
Source : DAWASA watakiwa kufanya kazi usiku na mchana, RC Makalla
Ukisikiliza ahadi mpya mpya zilivyokuwa tamu huku zikishadadiwa na takwimu luluki, unaweza kufikiri tatizo limekwisha kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. Kumbe hii ni kawaida yao, kila siku wanakuja na porojo hizi hizi.
 
Back
Top Bottom