Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Mnara huu upo kaskazini mashariki mwa Uwanja wa Taifa, ni mnara wa kumbukumbu ya marubani wawili wa ndege vita ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambao ndege yao ilianguka wakati wa maonyesho ya ndege hizo tarehe 01/09/1980.
Mara baada ya kuibuka na ushindi katika vita ya Kagera, wanajeshi wa Tanzania, waliandaliwa sherehe za kuwapongeza ambazo kwa Dar Es Salaam, zilifanyika uwanja wa Uhuru, na ndipo kukawa na maonyesho ya ndege vita.
Wakati wa maonyesho hayo, ikatokea hitalafu katika ndege moja wapo, hivyo kupeleka marubani wa ndege hiyo kushindwa kui-control.
Ndipo walipochukua uamuzi wa kishujaa kwa kuamua kuielekezea ndege hiyo nje ya uwanja ili kuepusha umati wa raia waliojitokeza kuwalaki mashujaa wao wasipatwe madhila hayo.
Marubani wale wakafa kishujaa, na mnara ukawekwa kama kukumbuka ushujaa wao! Walipambana vitani wakafia kwenye sherehe! Nitaleta majina yao hapo baadae!
Daima tunawakumbuka!