Ni Kweli Rais Magufuli ana Roho Mbaya?
Watu wengi humu wamekuwa wakisema maisha yalikuwa mazuri sana wakati wa awamu ya nne, siwezi kupinga ama kuafiki hilo kwa kuwa sifahamu maisha ya kila mtu yalivyokuwa kipindi hicho.
Ni vigumu kupima hali ya kimaisha nchini kwa kusikiliza maoni ya mtu moja mmoja hapa JF, hivyo inatubidi kutafuta kipimo kimoja ambacho tunaweza kukitumia kulinganisha vipindi hivyo viwili kuona kama kweli maisha yalikuwa mazuri (kwa kila mtu) ama la.
Wengi wanaopinga utawala huu wa awamu ya tano wamekuwa wakisema kuwa JPM ameharibu uchumi, pesa haionekani, na maneno mengi mengineyo. Ni vigumu kujua ukweli lakini kwa kutumia kipimo cha wapenzi wa mpira wa miguu tunaweza kupata ukweli.
Uwanja wa Taifa umekuwa ukitumika kwa muda sasa, cha kushangaza wakati wa "neema" (kipindi cha JK) wakati watu walikuwa na pesa, uwanja huo haukuwahi kujaa. Nakumbuka wakati timu kubwa kabisa duniani ya Brazil ilipokuja kucheza hapo uwanjani mwaka 2010 watu hawakujaza uwanja kabisa, tena wakati huo ulikuwa bado mpya.
Lakini leo hii Simba wakicheza uwanja huo unajaa, kama hali ni mbaya kiasi hicho, hawa watu wanapata wapi pesa? Kama huyu Rais ni mbaya na analeta umasikini inakuwaje leo watu wengi wanaweza kulipa viingilio na kuujaza uwanja?
2019 Simba vs AS Vita
2012 - Simba vs Yanga
Naombeni majibu.