Mnataka Rais Samia awe mkali na mbabe, kwani anaongoza mbuzi?

Mimi nimeelewa vipengele vyote kasoro hapo kwenye kuongoza kwa kupokea maelekezo kutok kundi la watu nimeingia chaka kabisaa nipo Kigali narudi wiki ijayo hali tete
 
Mi ninavyojua yote ni mipango ya Mungu kwa Tanzania,maana Mungu alitujua kabla hatujazaliwa na anafikiria na kuchambua tunayoyawaza au tulioyawaza
 
Pale ambapo majambazi,wezi na vibaka watatapakaa mitaani, mawaka ya tigo,mpesa,airtemoney watapokonya hela na jua linawaka,, ndio mtoa post akili zitamrudi. Degree uchwara ni aibu kwa taifa
 
Cheka na nyani uvune mabuwa? Ndipo madawa ya kulevya wakauzwa mpaka mashuleni, mateja, ubakaji, mauaji ya vikongwe, viwanja vya ndege,bandarini, kubaki magenge wa madawa, twiga ,madini kupakiwa mchana. Mtoa maada ivi unajua developed nation kuna kitu deep state? Et USA, EU, China,
 
Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa. Mtoa mada nadhani hujaelewa kidogo juu ya jambo lenyewe lilivyo au ni kejeli.
Watanzania hawana shida na upole au ukali. Watanzania wasichotaka ni zile dalili za wazi kabisa za kutaka kuturudisha kwenye Enzi zile za ubabaishaji mwingi, upigaji, vitendo vingi vya kihalifu, ufisadi nk.
Watanzania wameshaoneshwa njia na CHUMA, kwa hiyo hawadanganyiki tena.
Tafakari, chukua hatua.
 
Maraisi wakali na madikteta wote walikuwa waroma (Catholics). Kwa sababu wamerithi utabaduni wa Roma ambao kiongozi wa dini huamrisha na aliye chini ni mtekelezaji.
 
Lini hayo mambo yalikosekana
 
Kwa hiyo mkuu enzi tunatawaliwa na liendazake Sisi tulikuwa mbuzi?
 

Chuma kilimfunga nani Kama sio Garagaja
 

Kwani sheria zinasemaje kuhusu hayo uliyoyasema??
 
Pale ambapo majambazi,wezi na vibaka watatapakaa mitaani, mawaka ya tigo,mpesa,airtemoney watapokonya hela na jua linawaka,, ndio mtoa post akili zitamrudi. Degree uchwara ni aibu kwa taifa

Kazi ya Raid unaijua lakini?

Unaijua kazi ya vyombo vya Dola?

Unaijua kazi ya mahakama?

Unaujua wajibu wa Raia?
 
Pale ambapo majambazi,wezi na vibaka watatapakaa mitaani, mawaka ya tigo,mpesa,airtemoney watapokonya hela na jua linawaka,, ndio mtoa post akili zitamrudi. Degree uchwara ni aibu kwa taifa
Ni wapuuzi kabisa! Pale uchumi utakapodhoofika kwa ufisadi,usimamizi mbaya wa rasilimali,ubadhirifu,ujangili na uzembe ndipo watakapopata akili! Baadhi ya watanzania wanadhani hii nchi ni kama Sweden,Uholanzi n.k kumbe hawajui bado ni nchi masikini inahitaji usimamizi mkubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…