MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Inasikitisha sana kuona kuna kundi kubwa la wapumbavu wanaowaandama hawa vijana wa kitanzania walioamua kutumia vipaji vyao kujipatia kipato kihalali. Wasanii wanajipambania ila wajinga wengi wanataka hawa vijana wajihusishe na siasa zao za majitaka. Mbaya zaidi kila siku ni kuwatukana kuwa hawajasoma.
Ni kweli wasanii wengi kama ilivyo wanamichezo wengi hawakusoma sana. Wengi waliishia darasa la 7 na kidato cha nne. Anawezaje kusoma sana wakati kwenye umri mdogo ndo kipaji kinaonekana zaidi? Mimi nilianza form one na mwenzetu mwanariadha ambaye aliishia muhula wa kwanza wa kidato cha pili. Tangu akiwa form one alishaanza trip za Ulaya. Kina Bow wow, hayati MJ, Thiery Henry na wengine wengi hawakufika mbali kielimu kutokana na vipaji. Kwa hiyo hata wasanii wetu ni hivyohivyo.
Ni kweli wasanii wana nguvu kubwa ya ushawishi kuliko sisi wengine. Mtu kama Diamond Platinumz ana ushawishi kuliko mawaziri na viongozi wengine wakubwa. Angekuwa pia na kipaji cha siasa angeweza kusumbua sana kama angetaka nafasi za kisiasa. Kina Diamond, Ally Kiba, Harmonize, Shilole wanajulikana na kila mtanzania ndani ya jamhuri ya Muungano. Ushawishi wao ni mkubwa mno.
Kikatiba wasanii wako sahihi kukisapoti na kujiunga na CCM. Hawajavunja sheria. Kuwalazimisha kusapoti itikadi wasizozitaka ni upunguani usioelezeka. Ninawasihi tuwaache hawa vijana wajitafutie riziki zao na sio kuwalazimisha upuuzi wa kujiunga na harakati majitaka za kina Mange, Lissu, Bagonza, na Maria.