Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Thread hii inasema alikuwa mtu mwema awekwe mahali pema. Malaika wanamchukua wanaenda mweka atulie.
Kabla hawajarudi inaandikwa nyingine ya kumponda na kusema alikuwa Shetani Malaika wanambeba tena wanamkimbiza Jehanamu.
Wakifika kule wanaibuka tena watetezi wake wanasema alitenda mema. Malaika wanatoka naye kumpeleka Mahali pema.
Imekuwa ni usumbufu mkubwa kwa Malaika na Mwendazake pia. Hajapata nafasi ya kupumzika kabisa.
Kaeni chini mkubaliane mwache usumbufu kwa ubishi usio na tija. Kubalianeni ijulikane akakae wapi mtu wa watu. Na si kuleta usumbufu kwake na kwa malaika.nao wanachoka kumbebelea na kukimbia kimbia naye kila wakati.