Mnawasumbua Malaika na Mwendazake huko aliko. Amueni moja ili naye atulizwe. Inaudhi sana

Mnawasumbua Malaika na Mwendazake huko aliko. Amueni moja ili naye atulizwe. Inaudhi sana

Imekuwa ni usumbufu mkubwa kwa Malaika na Mwendazake pia. Hajapata nafasi ya kupumzika kabisa.
Sasa mzee unataka akapumzike ili iweje?

Ule msemo bado unaendelea kazi kazi tu,
Ni mwendo wa ruti tu mzee.

Alafu, Wazee wa kanzu nyeupe wanasema " kama ulivyowafanyia wenzako na wewe utafanyiwa ivyo ivyo kwa kipimo kile kile".
 
Njia yake alishaitengeneza mwenyewe kulingana na matendo yake.

Malipo yake aliyapokea hapa hapa.
 
Thread hii inasema alikuwa mtu mwema awekwe mahali pema. Malaika wanamchukua wanaenda mweka atulie.

Kabla hawajarudi inaandikwa nyingine ya kumponda na kusema alikuwa Shetani Malaika wanambeba tena wanamkimbiza Jehanamu.

Wakifika kule wanaibuka tena watetezi wake wanasema alitenda mema. Malaika wanatoka naye kumpeleka Mahali pema.

Imekuwa ni usumbufu mkubwa kwa Malaika na Mwendazake pia. Hajapata nafasi ya kupumzika kabisa.

Kaeni chini mkubaliane mwache usumbufu kwa ubishi usio na tija. Kubalianeni ijulikane akakae wapi mtu wa watu. Na si kuleta usumbufu kwake na kwa malaika.nao wanachoka kumbebelea na kukimbia kimbia naye kila wakati.
kwamba malaika wanafanyakazi kwa kutusikiliza sisi
haya bhana
 
Nikisoma hii mizaha halafu nikawakumbuka wale 46 waliokufa uwanja wa Uhuru katika harakati za kuaga mwili wake nabakia na butwaa na mawazo mengi sana kuhusu nini hasa kinachoendelea kwenye akili za Watanzania wenzetu.

Yaani kuna idadi kubwa ya Watanzania walimuona Magufuli kama mtakatifu na mtume maalum aliyeletwa na Mungu kuwakomboa wanyonge toka mikononi mwa mafisadi na waoneaji. Hao 46 ni miongoni mwa hao, bila shaka.

Hapo hapo kuna idadi nyingine kubwa tu inamuona Magufuli kama shetani aliyeletwa kwa “bahati mbaya” na wazee wa CCM kuwatesa na kuwaua Watanzania huku akiendesha “upigaji” wa kiwango cha “SGR”! (Wanaojua hadithi ya Frankenstein’s monster inawiana na walichofanya wazee wa CCM hadi wao wenyewe waliishia kukikimbia au kukisujudu kiumbe chao ili kujiokoa na gadhabu yake).

Iweje watu tunaoishi nchi moja tupishane mtizamo kiasi hicho? Cha kushangaza zaidi ni kwamba makundi hayo mawili yana watu wa madaraja yote: kuanzia machinga hadi mabilionea; kuanzia darasa la saba hadi PhD; kuanzia vibarua hadi maDG; kuanzia walio uswahilini hadi walio uzunguni. Na makabila yote na dini zote!
 
Back
Top Bottom