Mnawasumbua Malaika na Mwendazake huko aliko. Amueni moja ili naye atulizwe. Inaudhi sana

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Thread hii inasema alikuwa mtu mwema awekwe mahali pema. Malaika wanamchukua wanaenda mweka atulie.

Kabla hawajarudi inaandikwa nyingine ya kumponda na kusema alikuwa Shetani Malaika wanambeba tena wanamkimbiza Jehanamu.

Wakifika kule wanaibuka tena watetezi wake wanasema alitenda mema. Malaika wanatoka naye kumpeleka Mahali pema.

Imekuwa ni usumbufu mkubwa kwa Malaika na Mwendazake pia. Hajapata nafasi ya kupumzika kabisa.

Kaeni chini mkubaliane mwache usumbufu kwa ubishi usio na tija. Kubalianeni ijulikane akakae wapi mtu wa watu. Na si kuleta usumbufu kwake na kwa malaika.nao wanachoka kumbebelea na kukimbia kimbia naye kila wakati.
 
Maoni ya wanadamu ndo yataamua uende wapi?..

As if Mungu mwenyewe haoni wala hajui matendo yetu Ila anasubiri maoni ya wengine
Waliobaki ili akupe hukumu??

Labda ndo maana kuna taasisi zinahangaika kutulazimisha tuwaone baadhi ya marehem ni watakatifu?..
 
Mkuu The Boss legeza misuli ya ubongo jamaa yupo katika comedy tu [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Najua ni comedy but hii dhana naiona ipo sana..
Watu hufikiri ukisifiwa Sana unapokufa utaenda peponi.
 
Hao watakuwa malaika wa buza ambao wanasubiri thread za jf kufanya maamuzi
 
Alikuwa ni mtu mwovu ata hittler anasubiri, waute malaika waovu waje kuchukua mtu wao, case closed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…