Mnawezaje kula mboga saba?

Mnawezaje kula mboga saba?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Sijawahi kuelewa kabisa mtu anakulaje ugali mboga saba kwa raha mustarehe akifurahia chakula, wengine wanaita kucheza drafti.

Mimi chakula kikizidi mboga tatu huwa naona kizunguzungu tu saa ya kula. Pia mboga zikiwa nyingi sana tofauti tofauti ugali huwa unawahi kuisha mboga zinabaki inabidi niendelee kula mboga tu. Tatizo linakuja kama mboga mmojawapo iliyobaki ni mlenda.

Mambo ya mboga saba yamekaa zaidi kama sifa za kijinga, ulafi, uharibifu wa chakula na kupoteza muda tu.
20240928_063416.jpg
 
tafsiri maana na sio maneno!.. mboga saba maana yake sio ulaji wa mboga saba ni mtu mwenye kujimudu kiuchumi ama mtu asiefukara hii ndo tafsiri yake...
 
View attachment 3109099
Kula matunda
 
20240928_063416.jpg

Kwetu hizi ni mboga za siku nzima na nyingine zitawekwa kwenye fridge
 
Sijawahi kuelewa kabisa mtu anakulaje ugali mboga saba kwa raha mustarehe akifurahia chakula, wengine wanaita kucheza drafti.

Mimi chakula kikizidi mboga tatu huwa naona kizunguzungu tu saa ya kula. Pia mboga zikiwa nyingi sana tofauti tofauti ugali huwa unawahi kuisha mboga zinabaki inabidi niendelee kula mboga tu. Tatizo linakuja kama mboga mmojawapo iliyobaki ni mlenda.

Mambo ya mboga saba yamekaa zaidi kama sifa za kijinga, ulafi, uharibifu wa chakula na kupoteza muda tu.
View attachment 3109099
Aiseee mimi maximum mboga tatu tu ikizidi hapo nitaacha nyingine.

Maharage+Mchicha(Tembele)+Roast Nyama au Samaki basi.
 
tafsiri maana na sio maneno!.. mboga saba maana yake sio ulaji wa mboga saba ni mtu mwenye kujimudu kiuchumi ama mtu asiefukara hii ndo tafsiri yake...
Msosi wa drafti mboga saba kujiseviaaa kwetu ngangari dona bamia weeeeeee - Triple 5 Babu.
 
Tulioishi pangu pakavu ndio ugali unaisha kabla ya mboga maana tulifunzwa kutokomba mboga, ukikomba ikaisha utakula ugali mkavu au na chumvi.

Waliozoea ndio hivyo mkuu, ugali kidogo mboga buku.
 
Wahindi ndo kiboko wana chakula chao kina mboga hata kumi na ushee ..mm hua naona km uchafu sasa. Maana raha ule mboga mbili basii....unakula samaki na nyama ...haiji !!Samaki nipe na mchicha chukuchuku...nyama nipe na tembele ..sasa unipe nyama,samaki kuku choma,mlenda,dagaaa,mchicha na maharage ???dah huko ni kuchafua tumbo..
 
Sijawahi kuelewa kabisa mtu anakulaje ugali mboga saba kwa raha mustarehe akifurahia chakula, wengine wanaita kucheza drafti.

Mimi chakula kikizidi mboga tatu huwa naona kizunguzungu tu saa ya kula. Pia mboga zikiwa nyingi sana tofauti tofauti ugali huwa unawahi kuisha mboga zinabaki inabidi niendelee kula mboga tu. Tatizo linakuja kama mboga mmojawapo iliyobaki ni mlenda.

Mambo ya mboga saba yamekaa zaidi kama sifa za kijinga, ulafi, uharibifu wa chakula na kupoteza muda tu.
View attachment 3109099
Kula kulingana na urefu wa kamba yako
 
Me yangu hata ikiwa mboga moja ila ni sharti viungo vifuatavyo niviweke

nyanya
hoho
kitunguu
karoti
nyanya chungu
biringanya
kiazi
embe

nachofanya ni kukatakata vipande vidogovidogo..alafu sivikaangi navitupia juu ya labda samaki sigeuzi vikiiva dakika 5 natoa
 
Wengine week nzima ni mboga Moja Ile Ile Mchana na usiku
 
Sijawahi kuelewa kabisa mtu anakulaje ugali mboga saba kwa raha mustarehe akifurahia chakula, wengine wanaita kucheza drafti.

Mimi chakula kikizidi mboga tatu huwa naona kizunguzungu tu saa ya kula. Pia mboga zikiwa nyingi sana tofauti tofauti ugali huwa unawahi kuisha mboga zinabaki inabidi niendelee kula mboga tu. Tatizo linakuja kama mboga mmojawapo iliyobaki ni mlenda.

Mambo ya mboga saba yamekaa zaidi kama sifa za kijinga, ulafi, uharibifu wa chakula na kupoteza muda tu.
View attachment 3109099
Mboga saba haina maana ule zote. Ni mini buffet nyumbani unachagua mboga uipendayo.
 
Back
Top Bottom