Mnayemfahamu au mlio karibu na H. Baba, msaidieni haraka sana - amekwama

Mnayemfahamu au mlio karibu na H. Baba, msaidieni haraka sana - amekwama

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Alifahamika kama mwanamuziki (sijui shughuli yake siku hizi).

Hivi karibuni ameibuka na mtindo wa kumshambulia mwanamuziki Diamond kwa kila anachofanya. Imefikia hatua hata ya kujilinganisha naye kwa anavyonunua. Inasikitisha!

Sielewi anafaidikaje au anakitafuta nini katika mashindano hayo na hata siioni dalili yoyote ya ye kuibuka mshindi ikiwa upande wa pili nao utaamua kuingia katika bifu. Mbaya zaidi, kwa tabia yake hii anamharibia hata Harmonize ambaye ameonesha heshima kubwa kwa bosi wake huyo wa zamani kupitia nyimbo zake.

Mlio karibu msaidieni huyo kijana, ajikite kwenye issues zake. Kama ana hasira sana na anahitaji kutuliza akili basi mwambieni kuna 'Dodo' mtaani huko aende akaisikilize atarudiwa na busara.

 
Alifahamika kama mwanamuziki (sijui shughuli yake siku hizi).

Hivi karibuni ameibuka na mtindo wa kumshambulia mwanamuziki Diamond kwa kila anachofanya imefikia hatua hata ya kujilinganisha nae kwa anavyonunua. Inasikitisha!

Sielewi anafaidikaje au anakitafuta nini katika mashindano hayo na hata siioni dalili yoyote ya ye kuibuka mshindi ikiwa upande wa pili nao utaamua kuingia katika bifu. mbaya zaidi kwa tabia yake hii anamharibia hata harmonize ambaye ameonyesha heshima kubwa kwa bosi wake huyo wa zamani kupitia nyimbo zake.

Mlio karibu msaidieni huyo kijana, ajikite kwenye issues zake kama ana hasira sana na anahitaji kutuliza akili basi mwambieni kuna 'dodo' mtaani huko aende akaisikilize atarudiwa na busara!!
 
Mm nadhani anashinikizwa na njaa au kuna shinikizo la mtu anamtuma!

[emoji117]kwann harmo au mgnt yake isimkataze kutumia jina la harmo au konde gang anapomsema boss w zaman wa mmakonde!?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Misukule On Freak.

Huyu Diamond aanzishe Dini Kabisa, Maana Inakuwaje Msukule Uumie Diamond Kutukanwa Wakati Yeye Mwenyewe Hasemi Kama Anaumia ?

Diamond/Wasafi wamemtumia sana Dudu Baya Kutukana na kudhalilisha watu kibao lakini sikuona msukule wowote unajitokeza kukemea.

Leo H Baba anawatukana Wasafi ( Kwa Kujipendekeza Kwake Kwa Harmonize Tu ) Mnaumia.

Jamaniee, Punguzeni Njaaaaa, Shobooo Na Kuabudu Watu Wenye Vijisenti.
 
Nimefungua huu uzi haraka nikizani amelazwa, au amekuwa omba omba au mtumiaji wa madawa, Nimesikitika sana kukuta kumbe habari yenyewe ya bifu. Hata simsaidii mie nasaidia kuelimisha watu wajikinge na Corona
 
Back
Top Bottom