Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 38,283
- 97,793
Ni nyumba za kisasa lakini bado hatuna mafundi wazuri wa kuweza kuzifanya ziendane na hali zote, zimekuwa ni nyumba nzuri sana kipindi cha kiangazi, kipindi cha mvua nyingi ni majanga matupu zinavuja mno lakini bado watu wanajenga sana nyumba kwa mtindo huo ambao sio rafiki hasa kipindi cha mvua.
Kuna mwenye nyumba hapa kila ikinyesha mvua lazima umuone fundi kapanda juu ya bati(navyotype tayari kuna fundi juu ya bati) na wapangaji wake wanalalamika sana maji kuingia ndani na kulowanisha vitu. Kila akiendelea kujenga style ni hiyo hiyo lawama nyingi akiziangushia kwa mafundi wake.
Mafundi upi ushauri wenu juu ya hili?
Upi ni mtindo mzuri wa kupaua nyumba kwa mazingira ya huku kwetu na aina ya mafundi tulionao mitaani?