Mnazipendea nini hidden roof house?

tatizo wabongo wanaiga sana. wanasema kwenda na fashion wenyewe. tunapanda hearsay .."flani kwake kafanya hivi na hivi", hatufanyi tafiti, tukiona dualis kesho kila mtu anataka dualis ..tukiona sienta kila mtu kesho anataka sienta.
Hili nalo ni tatizo kwenye jamii yetu ya kibongo, kwa sababu fulani kafanya acha na mimi nifanye, matokeo yake ndio hayo.
 
Swali lako umeshalijibu kwenye paragraph ya kwanza kwamba
"Ni nyumba za kisasa lakini bado hatuna mafundi wazuri wa kuweza kuzifanya ziendane na hali zote"
Kipi kifanyike ili kupata ubora halisi wa hizi nyumba? Nyumba unajenga haipiti hata mwaka inavuja
 
Hii ni hatari na nusu πŸ˜‚
 

Attachments

  • TikTok_7295804132701539589.mp4
    2.5 MB
Hapo juu imekaa kama beseni yani mvua ikinyesha inabeba maji kuingiza maji ndani ni rahisi hata kama kuna outlet ya kutolea maji, pia joto jua likpiga vizuri humo ndani hamkae bila ac
 
Hapo juu imekaa kama beseni yani mvua ikinyesha inabeba maji kuingiza maji ndani ni rahisi hata kama kuna outlet ya kutolea maji, pia joto jua likpiga vizuri humo ndani hamkae bila ac
Slop hapo ni shida kubwa pia, kwa joto kipindi cha joto kali ni tatizo.
 
Sasa iwe ni usiku, alafu hali kama hiyo inatokea. watoto watahangaika sana dah!.
Alafu kuwe na baridi inakera mno. Kuna jamaa alikuwa anasema kapasi zake nguo fresh tayari kwa interview siku inayofuata, mvua ikanyesha usiku anaamka asubuhi akakuta nguo zote zimelowana. Interview ikaishia hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…