GE2025 Mnec Mwaselela: Hakuna mtu aliyetumwa na kiongozi kutia nia ubunge na udiwani

GE2025 Mnec Mwaselela: Hakuna mtu aliyetumwa na kiongozi kutia nia ubunge na udiwani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM taifa Ndugu Ndele Mwaselela amesema hakuna mwanachama yeyote aliyetumwa na kiongozi wakitaifa wala mkoa kwenye mchakato wa kuchukua fomu za kutiania ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.

Mwaselela amewaambia waandishi wa habari kwamba kumekuwepo na maneno kua kuna baadhi ya watu wametumwa na viongozi kutiania kwenye kata na majimbo jambo ambalo si sahihi na nikinyume na msimamo wa chama na kauli ya mwenyekiti wa chama taifa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan hivyo watiania wasiwe na shaka waendelee kusubiri muongozo wa chama kama utakavyo elezwa na katibu wa chama mkoa kwa ngazi ya mkoa na katibu wa chama kata kwa ngazi ya kata pamoja na katibu mkuu wa chama taifa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Kuhusu uvumi wa yeye kuanchia ngazi hiyo ya MNEC na kwenda kugombea Mwaselela amesema kwa sasa hana mpango huo na hajachukua wala kurejesha fomu ya kutiania, kwakua kipaombele chake kikubwa kwa sasa ni kukitumikia chama katika kuhakikisha wanapata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi October mwaka huu, pamoja na kuwatumikia wananchi kwa kutatua changamoto zao.

 
Back
Top Bottom