GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kichwa cha Habari
MNH Je, na Sisi wenye Michogo mibaya kama Kona za Milima ya Senkeke mnapanga lini kutuandalia Ratiba zetu za Kuturekebisha
Daktari Bingwa wa Upasuaji Rekebishi na Upasuaji Urembo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Edwin Mrema, amesema kuwa Wataalamu wanafanya upasuaji kwa wagonjwa 12 hadi 15 kwa wiki , huku idadi kubwa ya wanaohitaji huduma ya Upasuaji rekebishi ikiwa ni wanaume wenye kipara.
Huduma zinazofanywa mara kwa mara ni pamoja na upasuaji rekebishi kwa majeruhi wa ajali za viwandani, barabarani, matukio ya moto; kukiwa na wastani wa wagonjwa sita hadi wanane kwa siku.
Dk. Mrema pia amesema mpaka sasa nchi ina wataalamu 10 ,waliobobea katika upasuaji rekebishi na upasuaji wa urembo.
Chanzo Taarifa: itvtz
Na hata Rafiki yangu nae Chogo Chemba mwenzangu Thierry Henry kasema nikijua Ratiba yenu nimpigie ili nae aje.