Ni swali ambalo nilitaka kuliuliza a while ago lakini naona huu ni wakati muafaka. Labda swali liulizwe kwanza kabisa yeye ni nani?
Nashauri watu wa-google na ku-yahoo jina hilo na kujionea wenyewe halafu turudi kulijibu hili swali.
Mzee Mwanakijiji, kwani Tanzania tunafanya due diligence?. Everything is possible.
Niliomba kajikazi fulani kwa wenzetu, kabla sijakubaliwa wakachukua details zangu zote mpaka biometric na kunicheki, japo nilikuwa cleared wakaniita tena na kutaka maelezo ya mambo fulani ya ajabu yaliyonitokea zamani, nikashangaa!, wenzetu wana details za kila kitu na wana keep records hakuna mfano!.
Ubalozi wa Uingereza huwa una despose properties zake nchini kidogo kidogo, properties hizo ziko kwenye prime area. Kuna tajiri mmoja, anaheshimika sana hapa nyumbani, alishinda bid ya kununua Kasri la Hammaton House alilokuia akiishi Gavana wa UK Zanzibar, next to nyumba ya Karume. Jamaa alikataliwa kuuziwa, kisa baada ya kushinda, walifanya due diligence, wakakuta not all his money ni clean money, wakamkatalia kata kata licha ya kutoa offer kubwa!.
Kama mimi tuu na wewe, tumeweza ku google na kuona madudu ya Ayobola Abiola, haiwezekani BOT hawakuyajua haya, wanajua kila kitu!. Maadamu UBA ni benki yao, mambo yao yanajulikana. Kwa sasa tuna benki 6 zenye Nigerian connection nchini na hata sijui sisi tuna biashara gani kubwa kihivyo na Naigeria hadi zilete benki zao!.
Ama kweli Tanzania ni shamba la bibi, kila mtu kujivunia na kujiondokea!