Mnijuze kuhusu Star times wadau!

Mnijuze kuhusu Star times wadau!

kwa mwendo huu hatutafika maana ni wizi mtupu!:juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle::juggle:
 
namba za ting ni zipi wadau ninataka kuchukua maana tv yangu ya itv ipo. Au ofisi zao ziko wapi? udN
 
Star times haina tatizo ni wewe tu!! ebu fungua channel 6 uangalie!!!!
TV Sibuka ina vipindi vizuri sana, ina movies kali sana ambazo huwezipata kwenye kituo kingine chochote cha TV, inaonyesha mechi live za ligi ya Uingereza na Ujerumani, UEFA nk. TV Sibuka ina kipindi cha hotuba Maridhawa za Mwl. Nyerere na viongozi wengine maarufu, kipindi cha jionee na vipindi vingi vya burudanai. Nadhani kuwa ukiiangalia TV Sibuka, utaipenda na utagundua kuwa fedha zako unazowalipa Star times zinalingana na unachokipata.
 
Whoever anayeiponda star times..ana jambo lake..mbona kuna channel za ukwel champions league ful kupitia sibuka au kbc, kuna mtv,bet,<music bbc,al-jazeera,tv france ,dscovery channel..na nyingine nyingi..na bado unalipa buku 9..
 
kwa sisi wapenda movies sta times ni upuuzi kabisa,nasubiri mwezi uishe niangalie ustaarabu mwingne..
 
Ting wanauza ving'amuzi vyao sehemu nyingi tu kuna pale Engen Mbezi Beach,hata pale nje ya Lutheran Church tangi bovu,pia wana mabango njiani hata pale Mwenge kwenda Mikocheni kwenye bajaji kuna bango lao,na Easy Tv wana mawakala wao kibao na mabango wapo Victoria,pale kwa Komba Mbezi Beach na Goigi kwa msomali adjacent na CRDB bank
 
Mjadala mzuri sana na muhimu huu hasa kwetu sie mikoa ambayo kesho tu tutafikiwa na hao jamaa wa Star na Ting...........lakini niko confused ipi bora hapo kabla sijaruka majivu na kukanyaga moto
 
Ting kaka startimes nimesha hama natumia DSTV now ila ni vzr ukachukuwa ting nimewahi kutumia startimes nikashishwa!
 
mnaongea hamuweki contact hamsaidiii kitu esp ting na easytv

Hata mimi nawashangaa wamebaki kelele tuuuuu! TING, TING, contacts hakuna nini maana yake jamani Hebu tuwekeeni hapa namba zao ili na sisi tulio mbali na Dar tuwatafute. Je! Wadau TING yenyewe inaonekana nchi nzima au nao ni kama hao Star Times maana tunasikia kwenye matangazo ni baadhi ya mikoa tu hasa ile miji mikuu kama Dar, Mwanza, Arusha n.k sasa sisi wa mikoani tunafanyaje wakuu?
 
Whoever anayeiponda star times..ana jambo lake..mbona kuna channel za ukwel champions league ful kupitia sibuka au kbc, kuna mtv,bet,<music bbc,al-jazeera,tv france ,dscovery channel..na nyingine nyingi..na bado unalipa buku 9..

Kweli mkuu, mtu analipa buku 9 anataka ale bata ya DSTV ya zaidi ya kilo.
 
Back
Top Bottom