HahahahaKitu pekee alichozidiwa Mwameja na Peter Manyika ni kuvaa kapelo
FAZA a.k.a Idd Pazi, umenikumbusha mbali sana aisee, kipindi hicho nina unazi wa mpira balaa, sio sasa.Mohamed Mwameja unaweza mshindanisha na faza, sio hawa wengine.
Huyo Golikipa wa Pan African enzi hizo, moja ya sifa zake kuu tulizokuwa tunazipata kitaa ni ya kuvuta bangi.JUMA PONDAMALI ndio baba lao.
Duh, umesema vyema, ingawa hapo kwenye u handsome kulikuwa na ulazima?...ingawa kweli jamaa amepanda alafu alikuwa brother man fulani hivi.Mwameja alikuwa sheedar. Uwezo wa Kipa huwa kwenye kuokoa one against one. Mwameja alikuwa bora zaidi kwenye eneo hilo. Aliokoa penalty nyingi na alikuwa anadaka moja kwa moja yaani kumeza au kuficha mashuti zaidi ya kuyapangua. Peter Manyika alikuwa mzuri kwenye purukushani mfano Kona n.k., alikuwa anaokoa kwa kupangua zaidi na hakuwa mzuri kwenye penalty.
Mwameja pia alikuwa na u-handsome fulani hivi, hivyo aliongeza mvuto.
Habari nyeti hii, nilikuwa naikumbuka kwa mbali sana, asante kutukumbusha.Mwameja huwezi kumfananisha na Peter Manyika. Mwameja alicheza kipindi ambacho Simba ilitamba pia katika mechi za kimataifa, hasa mwaka 1993. Mwameja aliinyima kwa kiasi kikubwa ushindi timu hatari kutoka Angola iliyokuwa ikijulikana kama ASA, yaani Atletico Sportive Aviacao, ikiwa na winga hatari kabisa Libengue, na wachezaji maarufu kama vile kipa wao Kanka Vemba, Abilio, Arlindo, Kuleka, Lolo, Gito, Gerry na Libengue mwenyewe. Alizuia mabao ya wazi hasa waliporudiana kwao mjini Luanda na mechi iliisha 0-0 na Simba ilisonga hadi fainali ya kombe la CAF kwa jumla ya mabao 3-1 iliyoyapata Dar. Mechi nyingine ya maajabu ni ile ya ya kombe la Challenge kati Simba na El Mereikh ya Sudan ambapo zilikuwa katika kundi moja, Simba ikihitaji ushindi huku wenyeji El Mereikh wakihitaji walau sare. Mwameja aliokoa mabao ya wazi na hadi dakika za mwisho mwisho mambo yalikuwa 1-1, dakika ya 87 hivi Nteze John akaiandikia Simba bao la pili, taa zikazimwa, washabiki wakavamia uwanja na kuwapiga wachezaji na hasa Mwameja ambaye alishangilia bao la pili kwa kuwakatia kiuno washabiki wa Mereikh. Pambano lilivunjika na Simba wakalazimishwa wacheze tena kesho yake, wakajitoa maana walipigwa kweli kweli, na El Mereikh ikaingia kwa ushindi wa mezani na ikatakiwa ikutane na mahasimu wao El Hilal, na El Hilal wakajitoa kuungana na Simba kwa kusema kwamba hawawezi kucheza na timu iliyofungwa, yaani El Mereikh
😳😳😳Mwameja pia alikuwa na u-handsome fulani hivi, hivyo aliongeza mvuto.
Umeshapata jibuOut of topic: Mimi nawashangaa Madrid kumtaka Courtois wakati Navas ni zaidi ya Courtois. Labda kama wanaangalia vigezo vingine kama umri n.k.
Pondamali alikuwa karataker na dojo alilofundishiwa ni kwa sensei bobani wanasema alikuwa na black beltHuyo Golikipa wa Pan African enzi hizo, moja ya sifa zake kuu tulizokuwa tunazipata kitaa ni ya kuvuta bangi.
Nakumbuka tuliambiwa jamaa ni mbabe balaa, eti aliwahi kumshika Mbwa wa polisi akamchana mdomo kati kwa kati.
Wasifu mkuu wa Pondamali kitaani ilikuwa ni fujo fujo na ubabe kuliko hata nafasi yake ya golikipa.Pondamali alikuwa karataker na dojo alilofundishiwa ni kwa sensei bobani wanasema alikuwa na black belt