Mnijuze: Nani alikuwa bora kati ya Peter Manyika na Mohamed Mwameja?

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
JHHK.JPG

Wakuu wa hili jukwaa, haswa wale wakongwe katika soka, mje mtujuze nani alikuwa bora haswaa katika eneo la golikipa kati ya golikipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Peter Manyika na mlinda mlango wa zamani wa Simba na Taifa Stars Mohamed Mwameja?

Karibuni kwa mjadala
 
Mwameja alikuwa sheedar. Uwezo wa Kipa huwa kwenye kuokoa one against one. Mwameja alikuwa bora zaidi kwenye eneo hilo. Aliokoa penalty nyingi na alikuwa anadaka moja kwa moja yaani kumeza au kuficha mashuti zaidi ya kuyapangua. Peter Manyika alikuwa mzuri kwenye purukushani mfano Kona n.k., alikuwa anaokoa kwa kupangua zaidi na hakuwa mzuri kwenye penalty.

Mwameja pia alikuwa na u-handsome fulani hivi, hivyo aliongeza mvuto.
 
Hawa magwiji wamecheza mpira katika zama tofauti kwa hiyo inakuwa tabu kidogo kuwalinganisha.Ila kwa sisi tuliowashuhudia wote vipindi wakiwa juu ya ubora wao tunampa ushindi Mohammed Mwameja.Huyu jamaa alikuwa na commanding presence akiwa golini.Ilikuwa tabu zaidi kwa mastriker kumfunga.Hata zilipofikia penalt alikuwa na ni hodari sana wa kuzipangua.Kwa kipindi kirefu hatujapata mfano wa makipa kama Mwameja ambaye mastriker walijaa hofu kumuona kasimama golini.Nakumbuka wakati anachipukia Coastal Union,kipa namba moja alikuwa ni Hamisi Makene lkn walipokuwa wakiingia kwenye mikwaju ya penalt lazima aingizwe Mwameja.
 
Mwameja huwezi kumfananisha na Peter Manyika. Mwameja alicheza kipindi ambacho Simba ilitamba pia katika mechi za kimataifa, hasa mwaka 1993. Mwameja aliinyima kwa kiasi kikubwa ushindi timu hatari kutoka Angola iliyokuwa ikijulikana kama ASA, yaani Atletico Sportive Aviacao, ikiwa na winga hatari kabisa Libengue, na wachezaji maarufu kama vile kipa wao Kanka Vemba, Abilio, Arlindo, Kuleka, Lolo, Gito, Gerry na Libengue mwenyewe. Alizuia mabao ya wazi hasa waliporudiana kwao mjini Luanda na mechi iliisha 0-0 na Simba ilisonga hadi fainali ya kombe la CAF kwa jumla ya mabao 3-1 iliyoyapata Dar. Mechi nyingine ya maajabu ni ile ya ya kombe la Challenge kati Simba na El Mereikh ya Sudan ambapo zilikuwa katika kundi moja, Simba ikihitaji ushindi huku wenyeji El Mereikh wakihitaji walau sare. Mwameja aliokoa mabao ya wazi na hadi dakika za mwisho mwisho mambo yalikuwa 1-1, dakika ya 87 hivi Nteze John akaiandikia Simba bao la pili, taa zikazimwa, washabiki wakavamia uwanja na kuwapiga wachezaji na hasa Mwameja ambaye alishangilia bao la pili kwa kuwakatia kiuno washabiki wa Mereikh. Pambano lilivunjika na Simba wakalazimishwa wacheze tena kesho yake, wakajitoa maana walipigwa kweli kweli, na El Mereikh ikaingia kwa ushindi wa mezani na ikatakiwa ikutane na mahasimu wao El Hilal, na El Hilal wakajitoa kuungana na Simba kwa kusema kwamba hawawezi kucheza na timu iliyofungwa, yaani El Mereikh
 
Mwameja alikuwa sheedar. Uwezo wa Kipa huwa kwenye kuokoa one against one. Mwameja alikuwa bora zaidi kwenye eneo hilo. Aliokoa penalty nyingi na alikuwa anadaka moja kwa moja yaani kumeza au kuficha mashuti zaidi ya kuyapangua. Peter Manyika alikuwa mzuri kwenye purukushani mfano Kona n.k., alikuwa anaokoa kwa kupangua zaidi na hakuwa mzuri kwenye penalty.

Mwameja pia alikuwa na u-handsome fulani hivi, hivyo aliongeza mvuto.
Duh, umesema vyema, ingawa hapo kwenye u handsome kulikuwa na ulazima?...ingawa kweli jamaa amepanda alafu alikuwa brother man fulani hivi.
 
Mwameja huwezi kumfananisha na Peter Manyika. Mwameja alicheza kipindi ambacho Simba ilitamba pia katika mechi za kimataifa, hasa mwaka 1993. Mwameja aliinyima kwa kiasi kikubwa ushindi timu hatari kutoka Angola iliyokuwa ikijulikana kama ASA, yaani Atletico Sportive Aviacao, ikiwa na winga hatari kabisa Libengue, na wachezaji maarufu kama vile kipa wao Kanka Vemba, Abilio, Arlindo, Kuleka, Lolo, Gito, Gerry na Libengue mwenyewe. Alizuia mabao ya wazi hasa waliporudiana kwao mjini Luanda na mechi iliisha 0-0 na Simba ilisonga hadi fainali ya kombe la CAF kwa jumla ya mabao 3-1 iliyoyapata Dar. Mechi nyingine ya maajabu ni ile ya ya kombe la Challenge kati Simba na El Mereikh ya Sudan ambapo zilikuwa katika kundi moja, Simba ikihitaji ushindi huku wenyeji El Mereikh wakihitaji walau sare. Mwameja aliokoa mabao ya wazi na hadi dakika za mwisho mwisho mambo yalikuwa 1-1, dakika ya 87 hivi Nteze John akaiandikia Simba bao la pili, taa zikazimwa, washabiki wakavamia uwanja na kuwapiga wachezaji na hasa Mwameja ambaye alishangilia bao la pili kwa kuwakatia kiuno washabiki wa Mereikh. Pambano lilivunjika na Simba wakalazimishwa wacheze tena kesho yake, wakajitoa maana walipigwa kweli kweli, na El Mereikh ikaingia kwa ushindi wa mezani na ikatakiwa ikutane na mahasimu wao El Hilal, na El Hilal wakajitoa kuungana na Simba kwa kusema kwamba hawawezi kucheza na timu iliyofungwa, yaani El Mereikh
Habari nyeti hii, nilikuwa naikumbuka kwa mbali sana, asante kutukumbusha.
 
Huyo Golikipa wa Pan African enzi hizo, moja ya sifa zake kuu tulizokuwa tunazipata kitaa ni ya kuvuta bangi.

Nakumbuka tuliambiwa jamaa ni mbabe balaa, eti aliwahi kumshika Mbwa wa polisi akamchana mdomo kati kwa kati.
Pondamali alikuwa karataker na dojo alilofundishiwa ni kwa sensei bobani wanasema alikuwa na black belt
 
Back
Top Bottom