inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,344
- 21,967
kipa huwa mzuri akiwa na beki imara..unamaanisha mwameja hakuwahi kufungwa na timu zingine zaidi ya yanga!?..na kama alifungwa na nyota nyekundu au pilsner basi gulamali alihusika!!?..acheni hizo..mwameja kafungwa hadi na bule salehe wa amka ya nzega!!Kujaribu kumlinganisha Mwameja na Manyika ni sawa na kujaribu kulinganisha suruali na chupi.Mi ni shabiki mkubwa wa Yanga but Mwameja was something else ..Alikuwa hafungiki .Katika mechi ambazo Yanga ilimfunga Mwameja basi jua kilikuwa na mkono wa Gulamali
Kujaribu kumlinganisha Mwameja na Manyika ni sawa na kujaribu kulinganisha suruali na chupi.Mi ni shabiki mkubwa wa Yanga but Mwameja was something else ..Alikuwa hafungiki .Katika mechi ambazo Yanga ilimfunga Mwameja basi jua kilikuwa na mkono wa Gulamali[/Q afadhali hata wangemtaja Steven Nemes.manyika hamfikii hats often martin.
Wasifu mkuu wa Pondamali kitaani ilikuwa ni fujo fujo na ubabe kuliko hata nafasi yake ya golikipa.
Mkuu embu endelea, malizia Mkuu...Mwameja huwezi kumfananisha na Peter Manyika. Mwameja alicheza kipindi ambacho Simba ilitamba pia katika mechi za kimataifa, hasa mwaka 1993. Mwameja aliinyima kwa kiasi kikubwa ushindi timu hatari kutoka Angola iliyokuwa ikijulikana kama ASA, yaani Atletico Sportive Aviacao, ikiwa na winga hatari kabisa Libengue, na wachezaji maarufu kama vile kipa wao Kanka Vemba, Abilio, Arlindo, Kuleka, Lolo, Gito, Gerry na Libengue mwenyewe. Alizuia mabao ya wazi hasa waliporudiana kwao mjini Luanda na mechi iliisha 0-0 na Simba ilisonga hadi fainali ya kombe la CAF kwa jumla ya mabao 3-1 iliyoyapata Dar. Mechi nyingine ya maajabu ni ile ya ya kombe la Challenge kati Simba na El Mereikh ya Sudan ambapo zilikuwa katika kundi moja, Simba ikihitaji ushindi huku wenyeji El Mereikh wakihitaji walau sare. Mwameja aliokoa mabao ya wazi na hadi dakika za mwisho mwisho mambo yalikuwa 1-1, dakika ya 87 hivi Nteze John akaiandikia Simba bao la pili, taa zikazimwa, washabiki wakavamia uwanja na kuwapiga wachezaji na hasa Mwameja ambaye alishangilia bao la pili kwa kuwakatia kiuno washabiki wa Mereikh. Pambano lilivunjika na Simba wakalazimishwa wacheze tena kesho yake, wakajitoa maana walipigwa kweli kweli, na El Mereikh ikaingia kwa ushindi wa mezani na ikatakiwa ikutane na mahasimu wao El Hilal, na El Hilal wakajitoa kuungana na Simba kwa kusema kwamba hawawezi kucheza na timu iliyofungwa, yaani El Mereikh
Ha ha haa! Siku ile ya El Mereikh pambano lilikuwa kali ni balaa! Hata hilo goli moja walilopata El Mereikh hakika halikuwa bao, kwani mpira wa faulo uliopigwa na mchezaji wa El Mereikh uliingia kupitia wavu mdogo wa pembeni ukitokea nje, lakini mwamuzi Juma Ali David wa Zanzibar akaona tu mpira upo wavuni, akaweka kati! Haikuwa rahisi kwa Simba ile ya Mwameja kukubali goli hivi hivi, kwani mpira ulisimama kwa zaidi ya dakika tano Simba wakipinga goli, huku Mwameja akiwa kiongozi wa kukataa bao, huku akiwa ameukumbatia mpira (ukiwa mmoja uwanjani) akikataa usiwekwe kati. Akiwa amejisahau, Ramadhani Lenny Kaingilila Maufi akauchukua na kuanza kuupeleka kati, Mwameja akashtuka kuona uelekeo wa Lenny, akamkombiza na kumkaba kisha kuuchukua tena, kuendeleza ubishi. Baadaye joto likapoa Simba wakakubali liwe goli tu. Hata hiyo faulo ilitokana na nidhamu mbovu ya Mwameja, maana alikuwa ameudaka, akataka kuupiga mbele lakini mchezaji mmoja wa Mereikh akawa anazuia zuia kila mara. Basi Mwameja akasogea kidogo akaupiga mbele na kuusindikiza mguu (teke) kwa mchezaji huyo. Refarii Juma Ali David akaamuru ipigwe faulo, na kwa kuwa ilikuwa karibu na lango, wachezaji kama sita walijipanga kwenye mstari wa goli halafu wakamweka Mwameja mbele yao!Mkuu embu endelea, malizia Mkuu...
kipa mzuri ni mzuri tu mkuu, hakuna suala la beki wala nini, mfano mzuri ni david de gea wa manchester utdkipa huwa mzuri akiwa na beki imara..unamaanisha mwameja hakuwahi kufungwa na timu zingine zaidi ya yanga!?..na kama alifungwa na nyota nyekundu au pilsner basi gulamali alihusika!!?..acheni hizo..mwameja kafungwa hadi na bule salehe wa amka ya nzega!!
simba mwenzangu hapa kwa Aishi nakataaaaMakipa hatari kwa mfuatano na umaarufu ni Juma Pondamali,Mwameja, Kaseja na sasa Aishi
Mkuu sikupingi ila nauliza tu, hivi kipindi Stella Abijan wakiifunga simba na Bolizozo akawa maarufu zaidi ya raisi wa Tz golikipa wa Simba alikuwa nani?Mwameja huwezi kumfananisha na Peter Manyika. Mwameja alicheza kipindi ambacho Simba ilitamba pia katika mechi za kimataifa, hasa mwaka 1993. Mwameja aliinyima kwa kiasi kikubwa ushindi timu hatari kutoka Angola iliyokuwa ikijulikana kama ASA, yaani Atletico Sportive Aviacao, ikiwa na winga hatari kabisa Libengue, na wachezaji maarufu kama vile kipa wao Kanka Vemba, Abilio, Arlindo, Kuleka, Lolo, Gito, Gerry na Libengue mwenyewe. Alizuia mabao ya wazi hasa waliporudiana kwao mjini Luanda na mechi iliisha 0-0 na Simba ilisonga hadi fainali ya kombe la CAF kwa jumla ya mabao 3-1 iliyoyapata Dar. Mechi nyingine ya maajabu ni ile ya ya kombe la Challenge kati Simba na El Mereikh ya Sudan ambapo zilikuwa katika kundi moja, Simba ikihitaji ushindi huku wenyeji El Mereikh wakihitaji walau sare. Mwameja aliokoa mabao ya wazi na hadi dakika za mwisho mwisho mambo yalikuwa 1-1, dakika ya 87 hivi Nteze John akaiandikia Simba bao la pili, taa zikazimwa, washabiki wakavamia uwanja na kuwapiga wachezaji na hasa Mwameja ambaye alishangilia bao la pili kwa kuwakatia kiuno washabiki wa Mereikh. Pambano lilivunjika na Simba wakalazimishwa wacheze tena kesho yake, wakajitoa maana walipigwa kweli kweli, na El Mereikh ikaingia kwa ushindi wa mezani na ikatakiwa ikutane na mahasimu wao El Hilal, na El Hilal wakajitoa kuungana na Simba kwa kusema kwamba hawawezi kucheza na timu iliyofungwa, yaani El Mereikh