Dolphin had baby with a CowWakuu nimekutana nayo hii mtandaoni ni ya kweli? Je huyu ni mnyama gani
- Tunachokijua
- Kumekuwa na video ya sekunde 9 inasambaa mitandaoni ikidaiwa ni mnyama wa ajabu mwenye muonekano wa ng'ombe mwenye mapezi. Video hiyo imehusishwa na mitazamo ya kiimani huku wengine wakidai mnyama anayeonekana amezaliwa kutokana na mchanganyiko wa mbegu ya Dolphin na ng'ombe
Ufuatiliaji wa JamiiCheck.com umebaini kuwa video hii imehaririwa kwa kutumia Akili Mnemba (AI) kutokana na vigezo hivi:
1. Mijongeo ya mtu kuanzia sekunde ya 3 ndani ya video unaonesha ana miguu mitatu ambapo mguu mmoja unaangalia mbele na miwili nyuma
Mtu anayetembea akiwa na miguu mitatu
2. Rangi ya mavazi ya mtu anayetembea imebadilika ghafla huku miguu yake ikiwa imetazama nyuma.
Nguo ya anayetembea ikiwa na rangi nyeusi/ Dark blue
Nguo ya anayetembea ikiwa na rangi nyingine ghafla
3. Mnyama anayefanana na ng'ombe anapoteza sura yake na kufanana na mnyama Seal.
Mnyama akiwa anafaka kufanana
4. Mikono ya mtu anayeonekana kwenye video imenataka na kuingiliana
Mikono inayoonesha imeungana
Aidha kupitia nyenzo ya uhakiki ya TinyEye, video hii inaleta matokeo ya mnyama Seal.