SI KWELI Mnyama anayefanana na ng'ombe aonekana ufukweni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Dolphin had baby with a Cow

Wakuu nimekutana nayo hii mtandaoni ni ya kweli? Je huyu ni mnyama gani



Your browser is not able to display this video.
 
Tunachokijua
Kumekuwa na video ya sekunde 9 inasambaa mitandaoni ikidaiwa ni mnyama wa ajabu mwenye muonekano wa ng'ombe mwenye mapezi. Video hiyo imehusishwa na mitazamo ya kiimani huku wengine wakidai mnyama anayeonekana amezaliwa kutokana na mchanganyiko wa mbegu ya Dolphin na ng'ombe

Ufuatiliaji wa JamiiCheck.com umebaini kuwa video hii imehaririwa kwa kutumia Akili Mnemba (AI) kutokana na vigezo hivi:

1. Mijongeo ya mtu kuanzia sekunde ya 3 ndani ya video unaonesha ana miguu mitatu ambapo mguu mmoja unaangalia mbele na miwili nyuma


Mtu anayetembea akiwa na miguu mitatu

2. Rangi ya mavazi ya mtu anayetembea imebadilika ghafla huku miguu yake ikiwa imetazama nyuma.


Nguo ya anayetembea ikiwa na rangi nyeusi/ Dark blue


Nguo ya anayetembea ikiwa na rangi nyingine ghafla

3. Mnyama anayefanana na ng'ombe anapoteza sura yake na kufanana na mnyama Seal.


Mnyama akiwa anafaka kufanana

4. Mikono ya mtu anayeonekana kwenye video imenataka na kuingiliana

Mikono inayoonesha imeungana

Aidha kupitia nyenzo ya uhakiki ya TinyEye, video hii inaleta matokeo ya mnyama Seal.
Hii technology (AI) itasumbua sana watu wasio taka kusumbua akili zao kuyachambua mambo.

Tunashukuru uwepo wa Jukwaa JAMII CHECK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…