Mnyama mkali na katili anajutia baada ya kugundua amefanya kosa kubwa

Zacht

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2020
Posts
1,124
Reaction score
2,472
Baada ya kugundua swala aliyemuua alikuwa mjamzito, simba alimwondoa ndama ambaye bado hajazaliwa na kujaribu kumtikisa tena.



Tabia yake aliyo onyesha haikuwa kawaida kama simba wengine, simba huyo aliyefanya mauaji makubwa na ilionekana alikuwa amefadhaika sana na kile alichokuwa amefanya na aliendelea kutazama na kuzunguka kana kwamba anatafuta njia ya kumrudishia uhai wake




Alijaribu kula windo lake lakini ghafla akasimama. Alionekana kupoteza hamu ya kula. Kushikwa na huzuni alilala kando ya swala aliyekufa.



" Inahitaji akili kuwa na majuto"

Picha hizo zilirekodiwa na Gerry Van Der Walt ambaye ni mpiga picha wa wanyamapori.
 
Hifadhi gani alichukua picha?
 
Niliiona quora ila shida ngeli sasa... nafuu umetufasiria duh!
 
uongo mtupu simba huwa anakawaida ya kupumzika kila anapokamilisha windo lake
 
Kuna yule jamaa mfupi toka chato anazidiwa huruma na huyu mnyama mara 100
 
Ukiua uzao kesho yake utakula nini???wanyama pia hujiulizaga.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…