Mnyama Tena Mawindoni Leo.

Mnyama Tena Mawindoni Leo.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Salamu wanamichezo.
Leo ndo ile siku tuliyokua tukiisubiri kwa hamu sana, pale Mnyama mkali kabisa mwituni, Simba SC atakapokua akipambana na timu bora kabisa toka nchini Kenya, AFC Leopards mida ya saa 12 kamili usiku.
Ikumbukwe kua Simba SC ya msimu huu inauwezo wa kushiriki ligi kuu za Kenya, Uganda na Tanzania kwa wakati mmoja na pote ikachukua ubingwa, na hii inatokana na ubora na ukubwa wa kikosi chake kwa sasa. Hivyo kukosekana kwa baadhi ya wachezaji si pengo hata kidogo.
Mara ya mwisho Mnyama alipokutana na hao jamaa wa Kenya, wakiwa katika kiwango bora kabisa aliwagonga nne kavu.. Leo naiona mvua ya magoli.
Pia ule mchezo wa Timu ya Taifa ya Uganda a.k.a The Cranes dhidi ya wachezaji toka nchini Tanzania.. ambao utarushwa mbashara kupitia kituo cha ZBC 2 utauona live kupitia Big Screen iliyopo uwanjani.
Karibuni Taifa Stadium, Kwenye Show Ya Mnyama.
 
Simba timu ya kawaida sana acha porojo mkuu! Wale mafaza mliosajili baada ya mechi 10 tu hoi!
 
Mkuu ndo mana nikasema tuna kikosi kipana chenye uwezo wa kucheza ligi tatu kwa wakati mmoja. Hebu angalia timu ina benchi kama hili; Tshabalala; Mlipili; Ndemla; Mzamiru; Mo Ibrahimu; Niyonzima: Salamba n.k huogopi tu Mkuu? Kwenye kila nafasi tuna option zaidi ya 2.
 
Wa-mchangani Sembo bado unashabikia vibonde?
 
Mkuu ndo mana nikasema tuna kikosi kipana chenye uwezo wa kucheza ligi tatu kwa wakati mmoja. Hebu angalia timu ina benchi kama hili; Tshabalala; Mlipili; Ndemla; Mzamiru; Mo Ibrahimu; Niyonzima: Salamba n.k huogopi tu Mkuu? Kwenye kila nafasi tuna option zaidi ya 2.

Hili Benchi Ulilolitaja Hapa Haki Ya Nani Kwa Ubora Ni Sawa au Zaidi Ya Kikosi Cha Kwanza Cha Yanga.

THIS IS SIMBA
 
Acheni kutuwekea mataputapu yenu, tunaangalia timu ya Taifa
 
Salamu wanamichezo.
Leo ndo ile siku tuliyokua tukiisubiri kwa hamu sana, pale Mnyama mkali kabisa mwituni, Simba SC atakapokua akipambana na timu bora kabisa toka nchini Kenya, AFC Leopards mida ya saa 12 kamili usiku.
Ikumbukwe kua Simba SC ya msimu huu inauwezo wa kushiriki ligi kuu za Kenya, Uganda na Tanzania kwa wakati mmoja na pote ikachukua ubingwa, na hii inatokana na ubora na ukubwa wa kikosi chake kwa sasa. Hivyo kukosekana kwa baadhi ya wachezaji si pengo hata kidogo.
Mara ya mwisho Mnyama alipokutana na hao jamaa wa Kenya, wakiwa katika kiwango bora kabisa aliwagonga nne kavu.. Leo naiona mvua ya magoli.
Pia ule mchezo wa Timu ya Taifa ya Uganda a.k.a The Cranes dhidi ya wachezaji toka nchini Tanzania.. ambao utarushwa mbashara kupitia kituo cha ZBC 2 utauona live kupitia Big Screen iliyopo uwanjani.
Karibuni Taifa Stadium, Kwenye Show Ya Mnyama.
Kuna msimu ulipoteaga humu we jamaa tukahisi kuna tatizo, kumbe upo
 
Back
Top Bottom