Pre GE2025 Mnyika alivyowatambulisha wagombea CHADEMA Mkutano wa Baraza Kuu, ukumbi walipuka alipotajwa Lissu

Pre GE2025 Mnyika alivyowatambulisha wagombea CHADEMA Mkutano wa Baraza Kuu, ukumbi walipuka alipotajwa Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Januari 20, 2025 ulilipuka kwa shangwe kutoka kwa wajumbe wa mkutano wa Baraza Kuu la Chadema unaoendelea baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, kuwatambulisha wagombea wa ngazi ya juu ya uongozi wa chama hicho.

Mnyika amewataja wagombea hao kuwa ni Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Charles Odero ambao wanawania nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema taifa, wengine ni John Heche, Mathayo Gekulu, Ezekia Wenje, Hafidh Salehe, Said Mohammed, Said Said na Suleiman Issa.

Mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wanaoingia kwenye mkutano wa baraza kuu la chama hicho.
 
Mlipuko si idadi ya kura, usiende na matokeo yako kesho hatutaki watu waishie mloganzila kwa presha afu mseme Mbowe aliweka AC ukumbini zenye viatarishi kwa wajumbe wa Lissu pekee.
 
Back
Top Bottom