SI KWELI Mnyika ameamua kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CHADEMA

SI KWELI Mnyika ameamua kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CHADEMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Mnyika21.Feb2026.jpg
 
Tunachokijua
John Mnyika ni katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Tanzania (CHADEMA), Aliyeteuliwa kuendelea kutumikia nafasi hiyo mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho January, 2025 ambapo Tundu Lissu aliibuka kidedea akimshinda aliyekuwa mshindani wake Freeman Mbowe.


Madai

Kumekuwapo na Taarifa inayosambazwa mtandaoni kwa kutumia grafiki zenye utambulisho wa Jambo TV kuwa John Mnyika amesema ameamua kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CHADEMA.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa inayomnukuu au Mnyika mwenyewe kuchapisha taarifa hiyo.

Akizungumzia uhalisia wa taarifa hiyo, Mnyika amesema si ya kweli bali imetengenezwa, akisisitiza kuwa hajawahi kusema chochote kilichonukuliwa kwenye grafiki hiyo.

Kdhalika Februari 20, 2026 kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Jambo TV haijachapisha taarifa hiyo bali wapotoshaji wametumia utambulisho huo kusambaza taarifa isiyo na msingi wa ukweli.
​
Back
Top Bottom