John Mnyika ni katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Tanzania (
CHADEMA), Aliyeteuliwa kuendelea kutumikia nafasi hiyo mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho January, 2025 ambapo
Tundu Lissu aliibuka kidedea akimshinda aliyekuwa mshindani wake
Freeman Mbowe.
Madai
Kumekuwapo na Taarifa inayosambazwa mtandaoni kwa kutumia grafiki zenye utambulisho wa Jambo TV kuwa John Mnyika amesema ameamua kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CHADEMA.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa inayomnukuu au Mnyika mwenyewe kuchapisha taarifa hiyo.
Akizungumzia uhalisia wa taarifa hiyo, Mnyika amesema si ya kweli bali imetengenezwa, akisisitiza kuwa hajawahi kusema chochote kilichonukuliwa kwenye grafiki hiyo.
Kdhalika Februari 20, 2026 kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya
Jambo TV haijachapisha taarifa hiyo bali wapotoshaji wametumia utambulisho huo kusambaza taarifa isiyo na msingi wa ukweli.