Wakuu nimekutana na hii, ina ukweli?
- Tunachokijua
- John John Mnyika ni Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo (CHADEMA) ambaye mbali na nafasi ya ukatibu Mkuu wa CHADEMA pia amewahi kuwa mbunge wa Ubungo, mwaka 2010-2025.
Mnamo Oktoba 8, 2024 imeibuka picha ya John John Mnyika ikiwa na maneno 'Wenetu wanahamasisha kujiandikisha sisi tupo Twitter' picha hiyo imetengenezwa na kuambatanishwa Nembo ya Wasafi Media ikimaanisha John John Mnyika ametamka maneno hayo. Picha hii iliibuka muda mfupi baada ya Mnyika kufanya Mkutano na Waandishi wa Habari (huu) akisisitiza Wanachama wa CHADEMA kujitokeza na kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 (Soma hapa).
Upi ukweli kuhusu picha hiyo?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa taarifa iliyobebwa na picha hiyo haina ukweli, nembo ya Wasafi Media iliyowekwa kwenye picha hiyo imetengenezwa na kufananishwa kwa makusudi ili kupotosha.
Kuhusu Nembo ya Wasafi
Uchambuzi wa JamiiCheck umebaini mapungufu kwenye Nembo ya Grafiki iliyotumika na kufananishwa na Wasafi Media. Aina ya maandishi iliyotumika (Font type) ni tofauti na maandishi yanayotumiwa na Wasafi Media katika kuchapisha taarifa katika kurasa zao mbalimbali.
Ukubwa wa Nembo ya Wasafi iliyotumika kwenye picha hiyo iliyoibuka ni tofauti na ukubwa wa Nembo unaotumiwa na Wasafi Media kwenye taarifa zao tazama hapa.
Aina ya Maandishi (Font) kutoka kwenye taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za Wasafi Media leo Oktoba 9, 2024
Aina ya Maandishi iliyotumika katika taarifa iliyoibuka kuhusu Mnyika Oktoba 8, 2024
Ukweli kuhusu maneno yaliyoandikwa kuhusu John Mnyika
JamiiCheck imefanya mawasiliano na John Mnyika ili kupata uhalisia wa maneno hayo yaliyoandikwa ambaye amekanusha na kusema maneno na taarifa hiyo siyo za kweli.