Mnyika amwaga radhi Magu

Mnyika amwaga radhi Magu

Wewe Ipole mbona unaropoka? watu wanatoapoint za maana wewe unakurupuka, oh, Mbowe ni kifisadi!!!! Toa point kwanza kisha umalizie na bifu lako na Mbowe. Hoja kwanza kama huna kaa kimya!!! Umeniudhi sana. By the way mimi si mshabiki wa Mbowe if you need to know
Siyo kulopoka ndugu yangu nimeeleza ukweli tu kama mutu alikopeshwa pesa NSSF hajarudisha paka leo kwanini asiitwe FISADI kinachokukera ni nini una share hapo kwa mbowe? au ni DJ mwenzio tueleze ili tufahamu
 
Sungusungu kwa watu wasioijua hasa kule kijijini ilikoanzia (acha mjini) ni jeshi la wananchi wenyewe walioamua kujilinda wenyewe dhidi ya maharamia wanaowaibia mali zao. Jeshi hili lilianzishwa kutokana na kukosa msaada wa jeshi la polisi wanapohitajika kulinda na kufuatilia mali za wananchi zilizoibiwa. Mwananchi yeyote ni askali wa jeshi la sungusungu ukiondoa watoto hasa wanosoma shule ya msingi. Ni jeshi lililofanikiwa kupunguza makali ya wizi wa mifugo hasa kanda ya magharibi na ziwa ambako hasa lilianzishwa miaka ya 80. Wananchi walikuwa wakiibiwa mifugo yao machana kweupe na wakitoa taarifa polisi wanakuja kwanza wamechelewa na hata hawafatilii hao wezi mpaka watu waliwajumuisha na wezi kwamba lao moja na ndipo wakaamua kujilinda wenyewe. Leo hii jeshi hili limekuwa ajira kwa baadhi ya vijana hasa ktk miji na kusababisha matatizo kwa wananchi wenyewe. Kusema na kweli hawa wanaolinda ktk miji kwa ujira na kuitwa sungusungu si sawa hawa ni kampuni ya ulinzi. Sungusungu ni kila raia wa eneo husika ni mwanajeshi na hawalipwi chochote ni kazi ya kujitolea.
 
Suala la msingi ni elimu ya uraia na masuala ya kisheria katika hili kundi watu mnapenda kwenda nje ya topic always kama mna personal bifu na mtu mkaazishe thread za bifu huko wengine tuendelee kupata nondo hapa endelea Kijana kutupa nondo
 
Wakuu,

Hivi hapo tatizo ni mgambo au ni sheria zetu? Ukiondoa Mgambo bado polisi wataendelea kunyanyasa raia. Ukiondoa polisi jeshi nao wataendelea.

Huwezi kutatua hilo tatizo kwa kufuta Mgambo au Sungusunga. Kinachotakiwa ni kutunga sheria zinazolinda haki za raia wetu na kuwaelemisha raia juu ya haki zao.

Mgambo na Sungusungu wakitumika vizuri wana faida kubwa sana.


Tatizo kubwa tulilo nalo hapa nyumbani ni kwamba hata wale wanaojidai wanazijua haki za kiraia, hawajijui kwamba hawazijui. Vinginevyo tungekuwa tumesikia jinsi wanavyoshiriki angalau kutuelimisha sisi ambao wanadhani hatuzijui.
 
Tatizo Nafikiri Ni Wana Elimu Gani Ya Kuitumia Kazini Zaidi Ya Kupewa Vijisent Watishie Wananchi Wapigie Ccm Siku Ya Mwisho....kazikwelikweli
 
Mnyika,

Fanyeni mipango ya kurekodi hizi speeches halafu mnaweka mp3 mtandaoni kiasi kwamba hata kama kuna mtu ana distort au kunahitajika clarifications mnampa link ya mp3 tu anapata verbatim.

Ila hatuwezi kuwa na neighbourhood watch iliyo effective kama elimu ya uraia ipo chini, hapo utakuwa una invite human rights abuses tu, kitu kinachotokea sasa hivi katika hizi militias za Sungusungu na Mgambo.

Wazo ni zuri Mkuu lakini naona wangeenda mbali kama wanataka kuwafikia na Wtz wa kawaida - ni bora kurekodi katika kanda na kuzisambaza au kuchezwa hadharani na wananchi wengi watasikia au wataweza kuzipata kwani wanaweza kumudu tape recorder kuliko MP3 mtandaoni.
 
naomba kujua maendeleo ya kimasomo ya Mnyika

najua wengine mtaona I am on his case lakini kwa umri wake i believe akipata elimu nzuri then anaweka kuwa kiongozi mzuri sana wa taifa letu.

Je mnyika uko University gani na unasomea nini
, na utamaliza lini?
 
Back
Top Bottom