Mnyika anafanya upotevu wa muda usiku uingie ili Dola imsaidie Mbowe. Hotuba yake ilipaswa kuwekwa kwenye vitabu

Mnyika anafanya upotevu wa muda usiku uingie ili Dola imsaidie Mbowe. Hotuba yake ilipaswa kuwekwa kwenye vitabu

Giza likishaingia hapo kizimkazi atampa mbowe assist, hatutaki mambo ya gizani!
 
Kama haya mambo yapo upinzani na kama tunatumia mabilioni ya pesa kulipa ruzuku na shughuli mbali mbali za kisiasa na uchaguzi, kwanini tusirudi kwenye system ya chama kimoja na hizo hela tukajenge barabara kwenye maeneo ambayo barabara hazifiki? Hii itatusaidia kupeleka maendeleo kwenye maeneo ya pembezoni.​
 
Huu ni uchochezi tu,lissu anamawakala wengi sana humo,waaminifu na wazalendo kwake, hivyo msihofu.
ila mbowe naye ana mawakala wengi zaidi kutoka kwa deep state ambao watamsaidia, hata nje ya ukumbi wa kupigia kura nasikia kuwa kuna difenda za polisi nyingi sana za kumlinda mbowe na kumsaidia pale itakapobidi
 
hivi mpaka sasa bado hawajaanza kupiga kura?
hapo tundu lisu ahesabie ameula wa chuya, hapati kitu.usiku ukiingia zoezi la kupiga kura litahujumiwa na kura zitaibiwa
Hivi milimani city inaweza iathiriwe na Giza kweli? Kama Kuna hujuma zimepangwa kufanywa hata ingekuwa mchana zingefanyika tu mkuu
 
Team Lisu hamna utulivu hata kidogo, uchaguzi uliisha fanyika, subirini matokeo.
 
ASKOFU AZUNGUMZIA UWEPO WA POLISI UCHAGUZI WA CHADEMA MLIMANI CITY.

Polisi wamejaa Mlimani City kwenye Uchaguzi wa CHADEMA. Lakini ni Polisi hao hao waliojaa Mahakama Kuu wakimzuia Askofu Mwamakula asiingie kusikiliza Kesi ya Ugaidi ya Mbowe. Ni mawakili Peter Kibatala, Jeremiah Mutobesya, Dickson Matata na wengine waliosisitiza kuwa Kesi haitaendelea bila Askofu kuingia. Kelele za wafuasi wa CHADEMA ziliongeza nguvu na Askofu akaingia mahakamani na aliendelea pia kihuhudhuria kila siku ya Kesi.

Ni Polisi hao hao walizuia magari wa BAVICHA mwaka jana yasifike Mbeya kwenye Mkutano wao na ni Polisi hao hao waliowapiga vijana na viongozi wa CHADEMA kule Mbeya wakiwemo Mnyika na Sugu. Pia walinyanyasa wanawake na kuwapiga bila aibu pia wakamuumiza kijana mmoja. Askofu Mwamakula alikuwa miongoni mwa watu waliopazia sauti jambo hili.

Ni Polisi hao hao waliozuia msafara wa Lissu pale Kibamba/Kiluvya Oktoba 2020 na nusura wamtandike kwa risasi Askofu Mwamakula alipoenda kumuona Lissu akuwa amezingirwa. Mungu hakuruhusu hilo litokee. Ni Polisi hao hao waliotuhumiwa kuua baadhi ya Wagombea wa CHADEMA katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na kuwasaidia Wagombea wa CCM watangazwe washindi hata kama pia hawakushinda. Polisi hao hao ambao walipiga mabomu Mbezi Luis kushinikiza mgombea wa CCM atangazwe, tukio lililomliza mtanganzaji wa kike.

Viongozi, wagombea, wajumbe na wanachama na wafuasi wa CHADEMA wawe makini na Nia ya uwepo wa Polisi wakiwa na silaha za moto katika Uchaguzi wao hapo Mlimani City kwani wasiwasi ni tahadhari nzuri. CHADEMA wasije wakafikiri kuwa Polisi, dola, Serikali na CCM wanajali sana usalama wao hao Mlimani City, bali wajue kuwa kuna maslahi yao wanalinda.

Kwa vyovyote vile, Askofu Mwamakula anatoa ushauri huu: Wajumbe wasiwaruhusu kuingia katika sehemu ya kuhesabia kura. Wajumbe wakipiga kura wasiondoke katika ukumbi hadi mshindi ametangazwa. Wanachama wengine wazunguke eneo lote la Mlimani City wakisubiri matokeo. Wasikubali kutishwa na Polisi au pia watu wengine kuwataka waondoke. Hii ni sauti ya Askofu aliyekuwa yuko karibu na CHADEMA wakati wa shida zao, hivyo inawatahadharisha.

Kama hilo Jeshi la Polisi lilishiriki kuwatangaza kwa nguvu wagombea wa CCM wakati ule wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 uwezekano pia upo wa kumtaganza kwa nguvu mgombea wa CHADEMA anayetakiwa na Serikali au CCM! Sisi Askofu tumekwisha kutimiza wajibu wetu wa kuwatahadharisha CHADEMA na umma pia!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 21 Januari 2025; saa 4:25 asubuhi
1737467635038.jpg
 
Back
Top Bottom