Mnyika: Jeshi la Polisi limkamate Kenani Kihongosi aelezee kikao cha CHADEMA kilikaa wapi kupanga vurugu

Mnyika: Jeshi la Polisi limkamate Kenani Kihongosi aelezee kikao cha CHADEMA kilikaa wapi kupanga vurugu

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

'Wamkamate Kihongosi akaieleze Polisi kikao cha siri cha CHADEMA kilikaa wapi kupanga vurugu' Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ameyasema haya Juni 17, 2026, kupitia mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya chama hicho Mikocheni, Dar es Salaam.

Aidha, John Mnyika, amekanusha madai kuwa Shilingi Milioni 900 zilizotolewa na wafadhili zitatumika kufadhili maandamano ya mwezi ujao, akisisitiza kuwa kauli hizo ni propaganda za uongo zinazosambazwa na kada wa CCM, Ally Hapi.

Mnyika ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano, Juni 17, 2026, ambapo ameweka wazi kuwa fedha hizo zilisharudishwa kwa wafadhili tangu Desemba mwaka jana baada ya chama kuwekewa zuio haramu la utendaji la siku 309, na kwamba zilikuwa maalum kwa ajili ya mradi wa jinsia na mafunzo ya uongozi kwa wanawake.

"Ally Hapi analeta propaganda za uongo kujaribu kuhusisha fedha hizo na maandalizi ya maandamano. CHADEMA si chama kinachovunja mikataba au kutafuna pesa za wadau. Fedha hizo hazitatumika kwenye maandamano; zilikuwa za mradi wa wanawake na utaratibu wa kuzirudisha kwa nchi husika ulishafanyika baada ya mradi kufika ukomo tukiwa kwenye zuio," amesema Mnyika.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa msaada wa fedha za nje ndani ya CHADEMA haufiki hata asilimia 2 ya bajeti yote, na kuitaka CCM nayo iweke wazi mamilioni inayopata kutoka kwa taasisi na vyama marafiki vya nchi za Magharibi na Mashariki badala ya kushambulia upinzani​
 
Jeshi lipi la polisi limkamate bosi wao? Jeshi ni la serikali, serikali ni ya CCM, CCM ndiyo chama tawala, Kihongosi atakamatwaje hapo?
 
Ccm ni chama mufilisi hawana hoja wala sera wamebaki kuteka na kuua pamoja na kuuza rasilimali za nchi hii kama njugu
 
Police
Msajili
Tuone Sasa Vumbi Likitimka Kumkamata Kenani Kihongosi (KK)
Kiwago Kikubwa Cha Shirika
 
Kihongosi anaongoza genge la vurugu na utekaji nchini.
 
Back
Top Bottom