Mnyika: Msajili Jaji Mutungi ameitisha kikao cha Makundi mbalimbali kujadili Katiba Mpya 26/5/2023, Sisi CHADEMA hatutaenda Hatuna Imani naye!

Mnyika: Msajili Jaji Mutungi ameitisha kikao cha Makundi mbalimbali kujadili Katiba Mpya 26/5/2023, Sisi CHADEMA hatutaenda Hatuna Imani naye!

Walitaka waitwa wao tu. Wapumbavu
Mkojo hakuna hata anayetaka kuitwa na huyo kibaraka, maana wala haamini kwenye suala la katiba mpya. Bila machafuko ni nadra kuandika katiba ya matakwa ya wananchi.
 
Katiba mpya sio ya chadema pekee nyie wengine nendeni mkajadili Tanzania tupate katiba nzuri
 
Usikatae wito kataa neno.
Kwa ushauri wangu wangeenda harafu kama ajenda kikao itaenda na kinyume cha matakwa yao hapo ndo wangekataa.
Lakini siyo kukataa wito.
Ni kipi kinashindikana kuweka mtu anayeaminika na wote? Mbona mtu kama Jaji Warioba wengi hawana tatizo naye? Kwani ni lazima kumuweka huyo anayefahamika wazi ni kibaraka, na hufuata chochote anachaombiwa na aliyemteua ili kulinda maslahi ya kundi fulani?
 
Siye chadema hatutashiriki hicho kikao Cha harusi, na si mnasema ukisusa nyie mwala ?? Basi nyie kuleni, sisi hatuwezi kula sumu.. hata mkila hamtashiba
 
Chadema mtapoteza kwa kujifanya special

Mngeenda msikilize afu mtoe nyongo zenu pale
 
Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika anesema amepokea Barua Kutoka kwa Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mutungi ikiwaalika kushiriki Mkutano wa kuratibu Katiba Mpya

Mnyika amesema Serikali imeamua Mutungi ndio ayaunganishe makundi yote nchini yaani Wafanyabiashara, Wasanii, Wakulima, Wafugaji, Wanasiasa nk katika maandalizi ya kuandaa Katiba Mpya

Mnyika amesema CHADEMA hawamwamini Jaji Mutungi kwa sababu ndiye Kiini cha Kupandikiza Migogoro hivyo hawatahudhuria Mkutano huo

Source: Mwanahalisi Digital

Msipoenda mtasimamisha mchakato? Maana mambo mengine ni magumu sana kuyaelewa. Nendeni, wekeni hja mbele ya meza. Kukataliwa au kukubaliwa hilo litakuwa sio jambo lenu. Mtatimiza wajibu.
Uongozi uko mmoja tu. Hakuna namna mtaukwepa.
 
Ungejibu na hizo id ulizotumia kudai hiyo katiba mpya, na sio hii ya uzandiki ya mwaka jana.
Huna lolote ulijualo. Katiba hiii tunaomba chadema wasiiinajisi kabisaaa, hiii ni katiba ya wananchi sio ya chama chenu.
 
Tumesema hatutashiriki , na hicho kikao hakuna kitakacho amliwa bila sisi chadema kuwepo ... hbr ndo hiyo
 
Huna lolote ulijualo. Katiba hiii tunaomba chadema wasiiinajisi kabisaaa, hiii ni katiba ya wananchi sio ya chama chenu.
Ni kweli, ila hamjawahi kudai katiba mpya. Na isitoshe ni nadra sana kuandika katiba mpya huku Afrika bila machafuko. Hiyo mnayotaka kuandika nyie ni ya kiccm zaidi.
 
Msipoenda mtasimamisha mchakato? Maana mambo mengine ni magumu sana kuyaelewa. Nendeni, wekeni hja mbele ya meza. Kukataliwa au kukubaliwa hilo litakuwa sio jambo lenu. Mtatimiza wajibu.
Uongozi uko mmoja tu. Hakuna namna mtaukwepa.

..Huenda hicho kikao ni mbinu nyingine ya kuchelewesha mchakato wa Katiba Mpya.

..Ngoja tuone kama Jaji Mutungi na wenzake kama wataleta matokeo mazuri.
 
Ni kweli, ila hamjawahi kudai katiba mpya. Na isitoshe ni nadra sana kuandika katiba mpya huku Afrika bila machafuko. Hiyo mnayotaka kuandika nyie ni ya kiccm zaidi.
Wananchi ndio walidai katiba myaa ndiomaaana ya walioba ikapatikana, kumbuka haikuwa takwa la vyama vya kisiasa, Bali wananchi ndio waliotaka katiba. Kwahiyo kikundi chenu kisinajisi kabisaa zoezi la upatikanaji wa katiba. Katiba Bora italetwa na wananchi wenyeweeee. Kwahyo kiambie kikundi chako kitulize mbwembwe na ngonjeraa. Tena kikae kimyaaa sisi wananchi tusio na mlengo wa siasa wa chama chochote tuwaleteee katiba itakayosimamia mstakabali wa vyama vyote vya kisiasa.
 
Mzee Rwaitama atafaa sana

..wako Majaji wa Mahakama ya Rufaa wa sasa na wa zamani wanaoaminika ambao wangeweza kuteuliwa kusimamia zoezi hilo.

..Tatizo Samia anasema anataka reforms na reconciliation halafu anaendelea kufanya kazi na watu kama Jaji Mutungi ambao wamehusika kutufikisha mahali hapa pabaya.
 
Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika anesema amepokea Barua Kutoka kwa Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mutungi ikiwaalika kushiriki Mkutano wa kuratibu Katiba Mpya

Mnyika amesema Serikali imeamua Mutungi ndio ayaunganishe makundi yote nchini yaani Wafanyabiashara, Wasanii, Wakulima, Wafugaji, Wanasiasa nk katika maandalizi ya kuandaa Katiba Mpya

Mnyika amesema CHADEMA hawamwamini Jaji Mutungi kwa sababu ndiye Kiini cha Kupandikiza Migogoro hivyo hawatahudhuria Mkutano huo

Source: Mwanahalisi Digital
Kwa kwa hakika wamepanga kushindwa! Dhamira njema haipo hata chembe!
 
Wenzao wakiendelea wasije kulalamika siku za baadaye.
Mtungi ni mtu mwovu. Wengine wakiamua kuendelea na mwovu, nao wanakuwa sehemu ya uovu.

Katiba ya nchi, halafu inasimamiwa na msajili wa vyama vya siasa, uliona wapi kitu kama hicho?

Kwenye hili Rais Samia amefeli. Washauri wa Rais, wasimpotoshe Rais. Mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa yanaishia kwa vyama vya siasa. Ni mamlaka gani msajili wa vyama vya siasa atayatumia kuyakutanisha makundi yote?
 
Back
Top Bottom