Pre GE2025 Mnyika: Mzee Kibao alitekwa na Kuuawa akiwa ametoka kuendesha Mafunzo ya Maandalizi ya Uchaguzi Serikali za Mitaa. Tutaendeleza Majukumu aliyoyaacha!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Katibu Mkuu wa Chadema mh Mnyika amesema Mjumbe wa sekretarieti ya Chadema hayati Ally Mohamed Kibao alitekwa na Kuuawa akiwa ametoka kuendesha Mafunzo ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Mnyika amesema wakati wanafuatilia Kwa karibu Wahusika wa Unyama huu ni Lazima waendelee na majukumu Yote waliyoachiwa na Meddy

Mnyika amesema ukurasani X

Baadae Mlale Unono🐼

==========

Mzee Ali Kibao alitekwa na kuuwawa akiwa ametoka kuendesha mafunzo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa mitaa, vijiji na vitongoji. Wakati tunachukua hatua mbalimbali kufuatia mauaji yake ni muhimu pia tuendeleze majukumu aliyoyaacha, mojawapo ni mafunzo ya viongozi wapya wa vijana wa Kanda na Mikoa. Waliomteka na kumuua naamini pamoja na udhalimu mwingine walilenga kupandikiza hofu na kuvuruga mipango @ChademaTz

Tuendelee kuonyesha kwa vitendo kuwa: hatuogopi na hatusimami; tunaendelea na mapambano ya haki.

Soma> Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Katibu Mkuu wa Chadema mh Mnyika amesema Mjumbe wa sekretarieti ya Chadema hayati Ally Mohamed Kibao alitekwa na Kuuawa akiwa ametoka kuendesha Mafunzo ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Somo gani alilokuwa akifundisha ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…