Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

ukihukumiwa na mahakama ukakata rufaa hutatumikia adhabu yako mpaka rufaa isikilizwe?
Tatizo au gumu uko wapi kuita hilo sijui baraza na kupiga muhuri wa mwisho. Mara nyingi watu wanakimbilia mifano ya mahakama. hawa sio criminals sio kesi ya jinai hapa ni kufuata taratibu za chama walizojiwekea kuita baraza kuu shida ni nini hapo kama ndio kikao cha mwisho cha kuamua rufaa.
 
Wafanyaje dola ipo chini ya CCM yote, mbona dikteta alitisha mpaka kwenye CCM?
Ndio maana nasema kama walikuwa wanamuogopa dikteta na sasa wanamuogopa Ndungai basi wasamehe na wakie kimya tu malalamiko yatasaidia nini wasitafute huruma hichi chama kikubwa kinatakiwa kuonesha ukubwa wake kama hili dogo linawashinda ya nchi watayaweza kweli.
 
Unakwenda police ukishakuwa na nakala ya barua. Kama huna unakwenda kufanya nini? Unajuaje ni nani ame sign ili kuweza kusema signature ime kuwa forged ? Inawezekana ina signature ya mmoja wa signatory wa chama.
 
Yale majina yalitumwa na polepole ndio mshangae nchi ilifika pabaya hii.
 
Hicho ki despatch ulichoweka ni cha CHadema cha NEC kiko wapi? alichosaini mtu wa CHadema? Mnajitekenya na kujichekesha wenyewe.Hako KA DESPATCH kenu mwaweza kuwa mumejisainia ofisini kwenu

NEC wakipokea kitu huwa wana despatch yao ya NEC iko wapi
Kwamba "NEC wakipokea kitu huwa wana despatch yao" Anayetakiwa kutoa despatch isainiwe ni nani, Ni yule aliyeleta barua/mzigo, AU yule aliyepokea??

Tuanzie hapo kwanza, labda mimi sielewi vizuri haya mambo, kwamba DHL au EMS wamekuletea parcel yako, halafu wewe uwape despatch yako waisaini!!!!! kweli??
 
Katibu mkuu wa Chadema J J Mnyika amesema ni miezi 5 imepita tangu amwandikie mkurugenzi wa uchaguzi NEC akitaka kujua ni nani alipeleka orodha ya majina ya akina Halima Mdee na wenzake na form zao zilisainiwa na nani pahala alipotakiwa kusaini Katibu mkuu.

J J Mnyika anashangazwa sana na ukimya wa NEC ambao walipokea barua yake tangu 27/11/2020

Ikumbukwe hapa tarehe 10/05/2021 Bawacha wanatimba bungeni kwenda kuwafurusha akina Halima Mdee na wenzake.

Kazi Iendelee!

Lazima wateme ndoano kina "mafedha" wasilete bla bla watu wanataka kujua walipata majina kutoka kwa nani?
 
Ndio maana nasema kama walikuwa wanamuogopa dikteta na sasa wanamuogopa Ndungai basi wasamehe na wakie kimya tu malalamiko yatasaidia nini wasitafute huruma hichi chama kikubwa kinatakiwa kuonesha ukubwa wake kama hili dogo linawashinda ya nchi watayaweza kweli.
Huna bunduki wala panga utafanya nini mbele ya mabomu? MUNGU atafanya kama alivyofanya kwa dikteta hakuna namna
 
Katika hili nadhani CHADEMA hawapo serious......baada ya miezi mitano ya kutojibiwa barua zenu mlifanya maamuzi gani....??
 
Tatizo au gumu uko wapi kuita hilo sijui baraza na kupiga muhuri wa mwisho. Mara nyingi watu wanakimbilia mifano ya mahakama. hawa sio criminals sio kesi ya jinai hapa ni kufuata taratibu za chama walizojiwekea kuita baraza kuu shida ni nini hapo kama ndio kikao cha mwisho cha kuamua rufaa.
Ndio hapo ushangae wanakwepa nini kuitisha baraza kuu limalizie? Wanapiga miyowe tu ohh kamatui kuu ikiamua ni kama mahakama.Toka lini maamuzi ya kamati kuu yakawa sawa na ya mahakama? Katiba inasema mtu anaruhusiwa kukata rufaa.Wao wamekata rufaa haya itisheni basi baraza kuu liamue.Wanakuwa bubu miezi mitano sasa wako bubu ,Kuna kitu wamekifanya akina Mnyika na MBOWE wake wanataka kusingizia kusiko husika
 
Hicho ki despatch ulichoweka ni cha CHadema cha NEC kiko wapi? alichosaini mtu wa CHadema? Mnajitekenya na kujichekesha wenyewe.Hako KA DESPATCH kenu mwaweza kuwa mumejisainia ofisini kwenu

NEC wakipokea kitu huwa wana despatch yao ya NEC iko wapi
Wewe ni msemaji wa NEC?
 
Hakuna mahakama hapa Tanzania, bali kuna majengo ya mahakama yanayoendeshwa na Makada wa ccm.
Kama mnajua hakuna mahakama, hakuna bunge vyote mali ya CCM wewe na Mnyika mnalialia nini mitandaoni!?.. nendeni kwa Samia ndo pa mwisho au waache akina Mdee wale pesa za ubunge.
 
Back
Top Bottom