Yamesemwa mengi kuhusu wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema. Sijui ni kwanini Chadema hawajifunzi, hawabadiliki? Viongozi wake wanafikiri migogoro kubishana bishana ndio siasa, hapana. Chadema ni chama kinachopendwa sana lkn uendeshaji wake kwa maana ya uongozi ndio shida. Viongozi wake wamekuwa watu wanaokaza shingo muda wote, hawataki kubadilika, hawataki kukubali yaishe ili maisha yaendelee, wanashikilia jambo lile lile hata kama halina manufaa yoyote. Kilichotokea katika uchaguzi wa 2020 kila mtu mwenye macho na masikio anafahamu hii sio siri! Maji yakimwagika hayazoleki! Baada ya uongozi wa Raisi Mama SASHA (Samia Suluhu Hassan) ni ukweli ulio wazi siasa za Tanzania zimekuwa za wazi na maelewano angalau, watu wameanza kuongea mambo kwa uwazi. Ningekuwa mimi ni kiongozi wa Chadema ningepiga moyo konde na kuanza upya kuepuka mapambano ndani ya chama. Wabunge hawa 19 mimi ningewasamehe kwani tatizo ni nini? Kwani wameua? Wote tunajua msimamo wa Chadema kuhusu tuhuma za EL kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015! Sasa kama Chadema waliweza kumkaribisha EL na kumupatia nafasi ya kugombea nafasi ya juu kabisa ya kiti cha uraisi 2015 wanashindwa nini kuwasamehe hawa wabunge 19? Misimamo ya baadhi ya hawa wabunge 19 inajulikana, kupambana kwao kunajulikana vizuri, wamefungwa gerezani, wamekaa sana mahabusu, wamepata kila adha ya misukosuko ya kisiasa, ni kwanini Chadema hawakumbuki yote haya na kuwasamehe hawa wabunge 19 ili maisha yaendelee na siasa nzuri na zenye hoja zianze? Mhe. Raisi Samia Suluhu Hassan (Mama SASHA) amekaribisha siasa za uweledi na ustaarabu na kuliunganisha taifa, ni kwanini Chadema hawajifunzi ili nao wakaleta maelewano ndani ya chama chao kwa kuzingatia ule usemi usemao "yaliyopita si ndwele tulonge yaliyopo na yajayo" sijui kama nimeukumbuka vizuri usemi huu, lakini lengo la usemi wenyewe ni kwamba tusonge mbele tuachane na yale yote yanayotukwaza!
CHADEMA ACHANA NA HAWA WABUNGE 19 TUJENGE TAIFA LETU PAMOJA.