MNYIKA ALIPELEKA MAJINA 19 YA WABUNGE WANAWAKE CHADEMA.
Na: Philipo Mwakibinga.
0758910403
Uongo ukizungumzwa mara nyingi lazima unaweza kufanana na ukweli lakini kamwe hauwezi kubadilika kuwa ukweli maana bado utakua ni uongo tu.
JOHN Mnyika anajitahidi sana kuhakikisha ndugu yake Halima Mdee na Wenzake wanaonekana waovu mbele ya CHADEMA kitu ambacho hakiwezi kuwa kama anavyotaka. Mnyika anazunguka kuhakikisha kila Kiongozi wa Wanawake CHADEMA Mkoa anatoa tamko ili kutaka kuonesha kuwa HALIMA MDEE na wenzake 19 hawapendwi lakini ukweli ni kuwa ameamua kujipa kazi kwa kusaliti kazi aliyoifanya yeye mwenyewe.
John Mnyika kama katibu Mkuu wa CHADEMA alitimiza jukumu lake la kisheria kupeleka majina ya Wabunge viti maalumu 19 ambao leo wanatusiwa na kubezwa kwasababu ya ukigeugeu wa Mnyika. Hakuna Mbunge aliyejipeleka kwa SPIKA kama baadhi ya BAWACHA na BAVICHA wanavyosema bali ni janja janja ya Mnyika kutaka kuonekana yukosafi japo kwa muda mfupi maana hatodumu na uongo wake siku zote.
TUME ya UCHAGUZI walipokea majina kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Mnyika kama sheria inavyotaka. Tatizo ni Mnyika alipogombezwa na akina Mbowe na John Mrema kuwa katika majina yale hakuna watu wao, ndipo aliamua kuwageuka akina HALIMA Mdee ili aweze kujikosha kwa akina Mbowe. Mbowe anjaua, Lema anajua na Lissu anajua pia, hata Mnyika yeye mwenyewe anajua.
Mdee na wenzake 19 ni Kondoo wa weusi wa kafara tu! Kama kujipeleka kuwa Mbunge wa viti maalumu ni rahisi kiasi hicho basi Suzani Kiwanga angekua Bungeni, kwanini wengine hawajajipeleka? Mnyika anamakosa makubwa sana kama katibu Mkuu kwakuwaacha Mdee 19 Washambuliwe wakati anajua ukweli wa Mungu kuwa yeye ndiye alipeleka majina yale na wale ndiyo Wabunge sahihi wa Viti Maalumu CHADEMA.
KWANINI HAWAENDI MAHAKAMANI? Kamwe Mnyika na CHADEMA yake hawana ujanjanja wa Kwenda mahakamani hata kidogo kwakua wanajua MAHELA atawaumbua. Wataendelea kupiga sarakasi lakini hawawezi kwenda mahakamani kwani ukweli unadhihiri. Wale msiyojua acheni kuwashambulia akina Mdee 19 hawana hatia ni TAMAA za Baadhi ya viongozi wa CHADEMA zimewafikisha hapa na kinachoendelea ni MZUGO TU anaofanya Mnyika kiwaadaa WANACHAMA WA CHADEMA ila siku wakijua! Duuu!