Mnyika anasema “Baada ya kutokea yaliyotokea nilikutana na Bulaya na wenzake ili dhamira yangu iniongoze, sawa wamekosea, lakini je, wapo tayari kutubu na kurudi?”
Anasema, “Nilichokigundua baada ya kufanya mazungumzo nao, mdomoni wanasema wanakipenda Chadema na wapo tayari kurudi na kushiriki kwenye chama, lakini tuwaachie ubunge. Binafsi nilichokigundua kinachowaweka bungeni ni masilahi ya ubunge pekee, hakuna kingine,”.
Ni wabunge wa Viti Maalumu waliofukuzwa Chadema kwa kukubali kuapishwa kinyume na maelekezo ya chama.
www.mwananchi.co.tz