Mnyika: Nyalandu na mwenzake ni wasaliti, wameshindwa kuvumilia baada ya mateso ya kuporwa ushindi wa ubunge mwaka 2020

Na bado, hawa ni kama kenge mpaka damu itoke masikioni ndio wanasikia
 
Vp kuhusu kina Gekul, Silinde, Waitara na wengineo??

Chadema siyo Chama cha mapambio. Ukihamia Chadema unafundishwa ukakamavu uvumilivu na ujasiri hakuna pambio. Sasa wale waimbaji wa mapambio lazima wakimbilie chama cha kusifu kuabudu ili waweze kuimba mapambio yao.
Jipe moyo man,huo ndo ukamanda kweri kweri'hiiiiiii,,,?
Chama kikosa intelijensia huwa kinalalamika baada ya madhara kutokea ya kupokea yeyote anaekuja mkihisi ni mwenzenu kumbe katumwa.
 
Hivi huyo mnyika hajawajua vizuri
Wanasiasa...leo yuko huku kesho yuko
Kule
Leo kasema hiki kesho anasema kile
Leo anakubali kesho anakata

Ova
 
Chadema kwisha habari yenu,Mlimfukuza Slaa na kumkumbati fisadi Lowossa kwa maneno ya kejeli eti chadema ni kama train kuna wanaopanda na kushuka njiani huku safari ikiendelea,hawakujua kuwa kashuka Kapten wa kuendesha chombo 😄😄😁Naye aliwaambia mmepakua choo mmekileta sebureni lazima kiwanukie tu, sasahivi chadema wameparanyika wote walikumbati wamewakimbia tena kwa kejeri kubwa, sasahivi wanatafuta maneno mepesi eti wananunuliwa, utafikiri ccm kununua imeanza leo kuna kipindi enzi za Slaa pale Arusha chadema ilikwisha fukuza madiwani watano,kwatuuma za kununuliwa na uchunguzi ukarudiwa wakachua viti vyote,Tokea kuondoka slaa hawajawai kushinda uchunguzi wowote wa marudio,ukiwaambia Slaa ndiye alikuwa injini ya Chadema wanatukana matusi,enti Mbowe ndio mpinzani wa kweli,Slaa anaondoka chadema aliacha wabunge zaidi ya 70 sasahivi chadema ina mbunge mmoja bado mnajipa matumaini kuwa Mbowe ni mwanasiasa mahili.Mwanasiasa gani mahili anayeshindwa kujua mtego wa adui yake? Mbowe kila mtu anayekuja kwake anaona sawa eti mtaji wa mwanasiasa ni watu,mpaka akaleta wakina Wema sepetu, chadema kidogo igeuke bongo movie 😁😁😄, Kifo cha chadema Mbowe anausika pakubwa asitafutwe mchawi.
Vp kuhusu kina Gekul, Silinde, Waitara na wengineo??

Chadema siyo Chama cha mapambio. Ukihamia Chadema unafundishwa ukakamavu uvumilivu na ujasiri hakuna pambio. Sasa wale waimbaji wa mapambio lazima wakimbilie chama cha kusifu kuabudu ili waweze kuimba mapambio yao.
 
Chadema In Blood

20210502_081302.jpg
 
Mnyika John akue sasa...asizungumzie kila tukio. Muhimu ni kufuata matakwa ya katiba ya chama kwa kilichotokea; aache kuzungumzia watu
 
Hata kesho ukisikia Nape kahamia upinzani,pasi na shaka atapewa na uongozi wa juu wa chama na vigeregere atapigiwa.
Siku akiamua kurudi CCM ataimbiwa nyimbo za umamluki na usaliti.
Hawa ndo wapinzani wa CCM hapa Tanzania.
Hivi utasemaje NYALANDU karudi CCM kwa kushindwa ubunge wakati alijiuzulu UBUNGE mwenyewe kwa hiari yake mwenyewe wakati anahamia CHADEMA?????
 
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho kilifahamu kuwa Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew, ambao wote walikuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, wangeondoka kutokana na mienendo yao waliyokuwa wakiionyesha kwa hivi karibuni.

“Hawa ni wasaliti, wamejiongeza wameshindwa kuvumilia baada ya mateso ya kuporwa ushindi wa ubunge mwaka 2020. Chadema itasonga mbele hadi mabadiliko, uhuru na haki na demokrasia vipatikane nchini.

“Mapengo yao yatazibwa na makamanda wengine na mapambano yanaendelea,” alisema Mnyika bila kutaka kufafanua kwa kina.

Juzi CCM iliwapokea Nyalandu na Mathew ambao ni makada wake wa zamani waliokihama chama hicho kati ya mwaka 2015 na 2017 na kwenda Chadema ambako hivi karibuni Nyalandu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kati na Mathew kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini.

Wawili hao walitangaza uamuzi huo katika mkutano mkuu maalumu wa CCM jijini Dodoma mbele ya Mwenyekiti mpya wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, huku wakiweka bayana masaibu waliyopitia na uamuzi wao huo wa kurejea kwenye chama tawala.

Nyalandu, aliyekuwa wa pili kutambulishwa na Rais Samia aliikana ahadi yake kutoihama Chadema ikiwa zimepita siku 1,278 tangu alipojiondoa CCM.

ADVERTISEMENT

Kwa nyakati tofauti, Nyalandu amekuwa akijinasibu kuwa hawezi kuihama Chadema, kwa mara ya kwanza alimtaka Machi mwaka 2019 akisema yeye hakwenda Chadema kwa mafuriko. Msingi wa kauli ulitokana na kitendo cha Edward Lowassa kurejea CCM akitokea Chadema.

Kama hiyo haitoshi, Nyalandu alirejea kauli hiyo Agosti 2020 kwa staili tofauti katika mkutano mkuu wa Chadema wa kuchagua jina moja la mgombea urais aliyepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita.

Katika mkutano huo, Nyalandu alishindwa na mpinzani wake, Tundu Lissu na baada ya matokeo kutangazwa aliwaondoa hofu wanachama wa Chadema kuhusu mapenzi yake ndani ya chama hicho, akisisitiza yupo pamoja nao.

Lakini, jana katika mkutano mkuu wa CCM akitumia staili ya kunukuu baadhi ya vifungu vya biblia Nyalandu alisema: “Hakuna furaha izidiyo furaha ya mtoto arejeapo nyumbani.

“Wimbo wa bwana hauimbiki katika nchi ya ugenini, Mzee Sumaye (Frederick), Lowassa (Edward) na Dk Slaa (Wilbroad) ni mashuhuda wachache kati ya wengi kwa nini wimbo wa bwana hauimbiki katika nchi ya ugenini. Nakupongeza Rais kwa uongozi wako shupavu, nakushukuru kwa kukubali kunipokea na kunisamehe pamoja na kuniruhusu kurejea chamani,” alisema Nyalandu ambaye ni wazari wa zamani wa Maliasili na Utalii.

Kwa upande wake, Mathew alisema: ‘‘Nimekuja hapa kusema neno moja, nimeamua kurudi nyumbani. Nilikuwa ndani ya CCM na niliondoka CCM. Lakini, kadri unavyoendelea kuwa nje ya Chama cha Mapinduzi basi unajihisi una upungufu, leo (jana) nina furaha kubwa ya kuja mbele yenu wajumbe wa mkutano mkuu na kamati kuu,” alisema Mathew, maarufu ‘Messi’ aliyewahi kuingia kwenye mikwaruzano na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020.

Sio katika uchaguzi mkuu tu, bali hata kwenye kura za maoni ndani ya CCM za mwaka 2015 ambazo Nape pia alimshinda Messi. Hatua hiyo ilizua sintofahamu na kuamua kutoka CCM kuhamia Chadema.
Sijui wanasiasa huwa mnawaonaga wananchi hawapambanui mambo ama!!

Yaani useme ulishawajua mienendo yao halafu huku tayari mliwapa uongozi huo wa kikanda kama mlishawajua mienendo yao ni yakisaliti mlishindwaje kuwavua nyazifa adi usubiri mtu aende kwingine ndo uanze bla bla!.
 
Seleman Mathew amerudi CCM kwasababu anajua Nape harudishwi na Chama kugombea Ubunge 2025.
 
"politics is who gets what and how"
 
Ninachokiona hao wanaokimbia ccm kwa kukosa cheo au nafasi kwenye majimbo watakimbilia ACT Wazalendo.

Chadema itawakataa na inatakiwa iwakatae ili IINUE Vijana wao wanaokipigania chama usiku na mchana.
 
Kuhama chama inakuwaje Ni usaliti? Binafsi sielewi hoja hizi za wapinzani.wakitoka ccm kwenda upinzani Sio wasaliti? Inasikitisha Sana chadema wanakuwa na fikra hizi wakati wanapigania demokrasia
 
Ninachokiona hao wanaokimbia ccm kwa kukosa cheo au nafasi kwenye majimbo watakimbilia ACT Wazalendo.

Chadema itawakataa na inatakiwa iwakatae ili IINUE Vijana wao wanaokipigania chama usiku na mchana.
Upinzani waache tabia ya kukumbatia wanaccm...wavune wasio na vyama hasa vijana
 
Back
Top Bottom