Pre GE2025 Mnyika: Tumealikwa Kwenye Kikao Cha kupitia Kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa lakini hatujapewa Rasimu, Wanachama tunaomba Ushauri wenu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatarejesha heshima ya box la kura.
Kama mnataka machafuko ili muingie madarakani mtakuwa mmeshashindwa siasa acheni mfanye mambo mengine.
 
Je kwa sheria iliyopitishwa majuzi ni nani mwenye jukumu la kuandaa uchaguzi wa serekali za mitaa, je ni kile kinachoitwa tume huru ya uchaguzi ama ni tamisemi? Kama kuna mkanganyiko tafutenis tafsiri mahakani, lakini msikatae wito.
 
Usikatae wito kataa unaloitiwa baada ya kuambiwa ukishaitika kama unaona sio

utapewa huko huko kama huzikubali kakatae huko huko baada ya kupewa
 
Honorable learned counsel and prominent journalist P.
I fully second your valuable opinion.
In consideration of the democracy transformation process which is cost-effective and as a matter of pre-determined polling results avoidance, both the general and local government elections must be merged and concurrently undertaken in 2025.

If this idea is implemented, political complaints shall be drastically minimized if not eliminated to safeguard the public interests; I can confidently assure you.
 
Mbona ccm wako madarakani kwa kumwaga damu za watu na inaonekana ni poa tu?
Inaonekana poa kwa kina nani?

Kama mnataka damu zimwagike mnazo sehemu za kuhifadhi wapendwa wenu wakati damu ikimwagika ?

Mwanasiasa yoyote anayewaza machafuko ndani ya nchi yake ni mwanasiasa wa hovyo hapaswi kupewa hata Kijiji.
 
Ushauri gani mnataka?

Nyie si mmesema mtaingia katika uchaguzi huku mazingira mazima ya uchaguzi yakiwa mabovu!.

Mtajijua wenyewe.

Tuliwaambia, Tuongozeni sisi wananchi tugomee na kupuuza uchaguzi huu feki , nyie mmekomaa tu na kutaka kuingia ktk uchaguzi huku kukiwa na kanuni na sheria mbovu.

Iko hivi, CCM watakupeni viti watakavyoamua kuwapa na wala siyo vile mtakavyoshinda!
 
Hata Zimbabwe enzi za Mugabe, na huko Sudan kwa Elibashir walikuwa wanasema kama ww, yaliyotokea ni historia.
Hali ikoje huko Sudan ?matokeo yake Al Bashir yuko salama zaidi kuliko waliofanya fujo atoke madarakani.

Msiombee hata siku moia CCM watoke kwa njia ya machafuko tujitahidi kupambana watoke kwa sanduku la kura tu.
 
Suluhisho ni nini? Tuwaache nyani watawale shamba la mahindi?
Ni watu wengi sana wanasema wasishiriki uchaguzi lakini kutoshiriki watakuwa wanampa CCM advantage kubwa sana na unaweza kuwa ndiyo mwisho wa CHADEMA. CCM anasurubiri kwa hamu mno wasusie ili aweke vyama bandia bungeni. Najua ni kweli kuwa kwa katiba hii CCM itapora tena ushindi lakini huwezi kujua... wananchi wanaweza kusema liwalo na liwe.
 
Inaonekana poa kwa kina nani?

Kama mnataka damu zimwagike mnazo sehemu za kuhifadhi wapendwa wenu wakati damu ikimwagika ?

Mwanasiasa yoyote anayewaza machafuko ndani ya nchi yake ni mwanasiasa wa hovyo hapaswi kupewa hata Kijiji.
Huo umwagaji wa damu kwa wapinzani uko chaguzi nyingi, ila kwakuwa ww unafaidika na huo uhayawani huwa unaona sawa tu.
 
Musikatae"WITO" hiyo ndio hekima, Mungu atawatangulia.
 
Mkuu tambua kuwa, hata binadamu akifikia umri mkubwa (kuanzia 80÷) , huanza kufanya mambo ya kitoto, na yeye huona yupo sahihi tu! Ndivyo ninavyo kiona chama changu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…