Mnyika: Viongozi waliokimbilia nje ya nchi sasa warudi nyumbani suala lao lilikuwa katika ajenda za Maridhiano

Mnyika: Viongozi waliokimbilia nje ya nchi sasa warudi nyumbani suala lao lilikuwa katika ajenda za Maridhiano

Kheee, wanarudi kwa tangazo la Mnyika? Si walisema hawarudi mpaka rais autangazie ulimwengu na kuwaomba kurudi, sasa imekuwaje tena?
Tangazo tayari kupitia wizara ya ulinzi mawaziri wako chini ya rais wetu mwema mama Samia(ukiangalia mihimili unaona wazi waziri anadondokea mhimili upi) ondoa shaka
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Viongozi na wanachama wao waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa na kiusalama sasa warudi nyumbani baada ya serikali kuwa imetoa tangazo bungeni

Mnyika amesema suala la viongozi hao wakimbizi lilikuwa moja ya ajenda ya Maridhiano

Mnyika amewataja Tundu Lissu, Lema na Wenje kuwa ni miongoni mwa walio nje ya nchi na Chama kitawaandikia rasmi kuwapa utaratibu wa kurejea nyumbani

Chanzo: ITV habari
Good warudi kwenye uwanja wa vita
 
Tatizo Lema na familia yake wameshanogewa na huko Canada.
 
Bila Mungu kuingilia kati haya maridhiano yasingefanyika. Karibuni nyumbani viongozi wetu
Kweli mkuuView attachment 2255016
FB_IMG_16530413371179364.jpg
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Viongozi na wanachama wao waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa na kiusalama sasa warudi nyumbani baada ya Serikali kuwa imetoa tangazo bungeni.

Mnyika amesema suala la viongozi hao wakimbizi lilikuwa moja ya ajenda ya Maridhiano.

Mnyika amewataja Tundu Lissu, Lema na Wenje kuwa ni miongoni mwa walio nje ya nchi na Chama kitawaandikia rasmi kuwapa utaratibu wa kurejea nyumbani

Chanzo: ITV habari
akili za chadema wanazijuwa wenyewe maana hawajulikani wanataka nini na hawataki nini?
lema alikimbia nini? alitishwa na nani? yaani mtu kakimbia kesi zake za utapeli na madeni mnamuita mkimbizi wa ki siasa?
 
Back
Top Bottom