zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Toka Rais Obama, mwenye asili ya Kenya kuchukuwa madaaraka makubwa duniani, kuwa Rais wa USA, Kenya imepiga hatua kubwa za wazi-wazi, kuanzia kwenye siasa, uchumi mpaka miundo mbinu.
Viongozi wa Kenya, kuanzia enzi za Kenyatta walikuwa ni wa kwanza kujilimbikizia mali, wao na familia zao, mtoto wa Kenyatta ni mmoja katika matajiri wakubwa sana Afrika na duniani na hakuna asiyejuwa kuwa utajiri huo wote si wa asili ni utajiri uliokuj baada ya baba'ke kuwa ni mwanasiasa na kiongozi na kuiba sana mali za Taifa na 10% kwa wingi katika kila aliyetaka yake yafanikiwe, hali kadhalika kwa Moi na viongozi wengine wote wa kisiasa wa Kenya.
Ingawa mrengo wao wa kiasa wa u "capitalism" uliwaruhusu kujilimbikizia mali, ilikuwa wakijilimbikizia mali bila kuijenga nchi yao vilivyo, walijitajirisha wao na familia zao na kulikuwa kuna ufa mkubwa sana kati ya matajiri (wengi wao wanasiasa) na masikini.
Yote hayo yameanza kubadilika toka ujio wa Obama, tunaiona Kenya ikijenga miundombinu mizuri na ya kisasa na tunaona ikizidi kupaa kiuchumi na kimataifa.
Jee, tutegemee wajomba zake Obama kutwaa madaraka?
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!