Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Rais Samia anastahili pongezi kwa aliyoyafanya

Kama mwanadamu ana mapungufu yake lakini tusisubiri afe ndio tumpongeze kwenye maisha yangu binafsi Sina deni kwake.Siku nikikutana nae nitatamani nimkumbatie nimwambie Asante sana.Sasa Sijui Mimi mwanaume watakubali wale machawa.Niliteseka sana na yule Dictator mwandazake.
 
Ameshindwa kulipa Wakandarasi toka mwaka wa fedha 2023/2024 miradi yote ya barabara na hiyo SGR imesimama
 
sijawahi kuekewa, hivi mtu anawezaje kuwa Christian halafu akamuomba Mungu ambariki muslim? …
 
Hayo aliyofanya ni mepesi mno hata wewe na njaa Yako ungefanya tu ili mradi unaitwa Rais. Hoja yetu sisi wengi, kwanini hatamki neno rushwa na ufisadi walau hata kukemea tu. Kila report ya ukaguzi fedha zimepigwa lakini hakuna kukemea wala hakuna action. Pili ni dhaifu mno na Hana creativity. Tatu ni silent dictator. Nne kakopa pesa nyingi lakini turn out ni ndogo. Mbaya zaidi hata pesa alizokopa amezikataa kwa kusema mikopo mingine ilikopwa awamu zilizopita na imekuja kutolewa awamu yake. 🤣. Sasa mtu kama huyu unasifu kwa lipi? Kama ni mnyonge huyu Bora anyongwe tu.
 
Pascal, achana na uchawa. Uchawa hauwezi kuwa na msaada wowote wa maana katika maisha yako.

kumbuka kuwa katika maisha ya mwanadamu, hakuna kilicho muhimu kuzidi uhai wake. Hata ufanye mazuri ya kiwango gani, lakini ukawa muuaji, au ukabariki mauaji, au ukapuuza uhai wa binadamu wenzako wanaouawa, mazuri yako yote yanafutika. Kwani hakuna zuri linalozidi uhai wa mwanadamu. Kwa upande wa serikali, jukumu la msingi la serikali yoyote makini Duniani, ni ulinzi wa uhai wa watu wake.

Mazuri yote ya huyu Rais yanafutwa na utekaji na mauaji ya wanaomkosoa, na udhulumaji mkubwa wa haki kwa ujumla, uliokithiri awamu hii. Rais hawezi kutenganishwa na utekaji na mauaji ya wanaomkosoa kwa sababu wakati wote ameyalinda matukio hayo kwa nguvu zake zote. Fikiria watu wanatekwa na kupotezwa, watu wanalalamika yeye anasema hakuna utekaji, kinachoitwa utekaji ni drama! Wanaomkosoa wanauawa, yeye anasema kifo ni kifo tu, yaani watu wasioni kutekwa na kuuawa ni kitu cha pekee.

Pascal ilitakiwa atekwe mwanao au mdogo wako, ukaione maiti yake mabwepande, ndiyo ungejua kuwa hakuna mbadala wa uhai.
 
Ningekwambia kuna mtu umfate ni rafiki wa Abdul wa karibu sana, toka Mama yake akiwa Makamu. Huku unauma na kupuliza haoni. Najaribu kuona unavyouzunguka mbuyu. Ila kabla ya kuchukua fomu, nenda kwenu kwanza, utakuja nishukuru.
 
Dah umekuwa chawa mchafu kwelikweli.eti serikali yake haihusiki na utekaji?yule bibi mzanzibar hana uchungu na watanganyika.mauaji yanayoendelea yana mbaraka wake
 
Unachukua form lini mkuu.
 
Hata Mimi namuunga mkono mh Rais kwa aliyoyafanya kwa nchi hii na kwa muda mfupi aliokaa mafarakani, wengine wanasema hana mradi mpya wa kwake na kusahau kuwa alikuwa na uwezo wa kuacha ya mtangulizi wake na kuanzisha yake,aheshimiwe kwa kumalizia hiyo miradi yote,nachoweza kusema ni hawa watendaji wa Chini ndio wanaomtukanisha Mh Rais ,mfano wa maji bomba kubwa la maji (nchi 4) linapita katikati ya miji bila kuwashirikisha watu wavute hata kwa kuchangia gharama za uchimbaji wa mitaro na vifaa,hilo huwezi kumlaumu Rais ni viongozi wa mamlaka za maji wamekosa ubunifu tu mbona watu wa mitandao ya simu kila siku wanabuni njia za kuvuta wateja,maoni yangu Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji wapimwe Kwa kuunganishia watu maji
 
Hivi haya yote yanayofanyika wewe mwenzetu huyaoni?
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…