Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Rais Samia anastahili pongezi kwa aliyoyafanya

W
Ni kweli Mafisadi,matapeli,vyeti feki na wauza ngada hawakuwa sehemu ya watanzania waliompenda Mwendazake...
Watu wameuza ngada na yeye Yupo.Ngada inauzwa mpaka kwa Trump.Hivi nyie mnafikiri wauza ngada kama wauza karanga.Hiyo biashara iliendelelea kama Kawa,na watu walipigwa vilevile.
 
Wewe jamaa hujijui kama umepoteza mvuto unaendelea kujaza seva tuu
 
Mahali popote mishe muhimu au mwenzetu unakula kwa Shemeji? Wafanyakazi wenyewe walitembelea choki.
Fanya kazi ya kueleweka! Acha habari ya mishe! Kama hujakoma, yatakuja makubwa kuliko ya JPM, au utaambukiza kizazi tabia ya misheni tauni.
 
Samia anafanya na amefanya mengi sana,kwa mtu asiyetaka kukubali huo ni ujinga wake,mama kafanya kazi kubwa mno,mimi huwa natembea sana nchi hii,aisee huyu mama kafanya makubwa
 
Kwa mazuri anastahili pongezi, kwa Yale mabaya anastahili lawama pia
 
Samia anafanya na amefanya mengi sana,kwa mtu asiyetaka kukubali huo ni ujinga wake,mama kafanya kazi kubwa mno,mimi huwa natembea sana nchi hii,aisee huyu mama kafanya makubwa
Kafanya makubwa kuweka mabango nchi nzima kupromoti wizi wake...
 
Kama unadhani hayo mabango barabarani ameyajaza yeye, endelea kudhani, mabango ya mabarabarani yamewekwa na waweka mabango na sio yeye!.
P
Wameweka kwa sababu wanajua ndicho anachokipenda.

Nikukumbushe Mayala:
Wakati wa awamu ya kwanza, kuna watu walianza mumwita Rais Nyerere, Musa, yaani wakimfananisha na nabii Musa aliyewatoa na kuwaongoza wana wa Israel toka utumwani Misri. Mwalimu Nyerere aling'aka, akasema, "mmeniita mchongameno, nimenyamaza, mmeniita haambiliki nimenyamaza, lakini hili la kuniita Musa, sitaki kulisikia tena", na baada ya pale hakuna aliyethubutu kumwita Musa.

Kuna wakati, kuna watu walianza kumwita Rais Nyerere, Mtukufu Rais Nyerere, Mwalimu Nyerere alikataa kuwa hataki kuitwa mtukufu wala mheshimiwa, mtukufu ni Mungu pekee yake, akataka yeye aitwe Ndugu, na ikawa hivyo.

Kwa hiyo Pascal, huwezi kumpata mjinga wa kuamini kuwa hayo mabango ya Samia yayowekwa kila mtaa, yamewekwa bila ya yeye kuhusika directly au indirectly. Hivi kwa uelewa wako, unaamini kwamba gharama ya kutengeneza hayo mabango imetoka mifukoni mwa watu binafsi? Kama ukiwa kiongozi responsible, huwezi kukubali kodi za wananchi ziibwe kwa kupitia mabango ya sura yako.
 
Aji
Ajira kwa vijana?

Mfumuko wa bei?


Dhamani ya shilingi?

Nakadharika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…